Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya akifungua kikao cha ushawishi cha Baraza la watoto wa manispaa ya Shinyanga na kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna leo Disema 21,2017. Kushoto ni Katibu wa kamati hiyo Raymond Kilindo ambaye ni Afisa Mipango wa manispaa ya Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Wajumbe wa Baraza la watoto manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya uchumi, elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga, Reuben Kitinya.
Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath akielezea lengo la kikao cha ushawishi kati ya wajumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga na wajumbe wa baraza la watoto manispaa ya Shinyanga.
Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath alisema shirika hilo kwa kushirikiana na serikali ya manispaa ya Shinyanga limeona ni vyema kuwapa nafasi watoto kueleza changamoto zinazowakabili mbele ya kamati hiyo
Mtoto Abdalah Said akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dossy akizungumza katika kikao hicho.
Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Shela Mshandete ambaye pia ni diwani wa viti maalum (CCM) akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa kamati ya uchumi, elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga, Moris Mugini ambaye ni diwani wa kata ya Chamaguha akizungumza katika kikao hicho.

Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga limefanya kikao cha ushawishi cha Baraza la watoto wa manispaa ya Shinyanga na kamati ya uchumi, elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga.

Kikao hicho kimefanyika leo Alhamis Desemba 21, 2017 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho, Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO, Shangwe Kimath alisema lengo ni kuwakutanisha watoto hao na wajumbe wa kamati hiyo ambao wanashiriki katika utengenezaji wa bajeti ya manispaa ya Shinyanga.

“Mradi wetu unatekelezwa katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na Kahama Mji,lakini leo tuna watoto wa manispaa ya Shinyanga,kupitia kikao hiki watoto wanaeleza changamoto wanazokutana nazo zinazopaswa kuchukuliwa hatua ngazi ya manispaa ikiwa ni pamoja na kushawishi bajeti ya manispaa iwe na mlengo wa kusaidia watoto”, alieleza Kimath.

Alisema kikao hicho cha kamati ya uchumi,elimu na afya na baraza hilo la watoto linaloundwa na watoto waliopo shuleni na ambao hawapo shuleni itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu ya ushawishi katika utengenezaji wa bajeti inayomlenga mtoto.

Wakizungumza katika kikao hicho watoto walizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na uhaba wa madarasa,walimu na watoto wa kike kukosa vifaa vya kutumia wakiwa katika hedhi hivyo kuomba serikali na mashirika mbalimbali kuangalia namna ya kutoa pedi kwa wanafunzi shuleni.

“Wanafunzi wa kike wamekuwa wakikosa masomo wanapokuwa katika hedhi,wanakosa pedi hivyo kuona aibu kufika shuleni lakini pia tunahitaji kila shule iwe na vyumba maalum vya kujihifadhi watoto wa kike wanapokuwa katika hedhi”, alieleza Nancy Aloyce kutoka Shule ya msingi Mwenge.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: