Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akizungumza wakati wa hafla ya Chakula cha usiku aliowaandalia Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes, iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni na kuwazawadia Fedha na Viwanja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi cheti ya shilingi miliono tatu Mchezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes Ibrahim Hamad Hilika.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheki ya shilingi milioni Tatu Nahodha Timu ya Zanzibar Heroes Suleiman Kassim Selembe, wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar katika ukumbi wa Zamani wa Baraza Kikwajuni.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheki Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Abdulazizi Makame, wakati wa hafla ya chakula cha usiku katika ukumbi wa Zamani wa Baraza Kikwajuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi cheki Kocha Mkuu wa Timu ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco
Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa kukabidhi zawadi kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes katika ukumbi wa zamani wa baraza kikwajuni Zanzibar
Wachezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes wakifuatilia hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhi Jezi ya Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Nahodha wa Timu hiyo Suleiman Kassim Selembe, wakati wa hafla maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar kuwazawadi zawadi wachezaji hao katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni.
Kocha Mkuu wa Timu ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati wa hafla maalumu ilioandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.Picha na Ikulu.
---
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa zawadi ya kiwanja kwa kila mchezaji wa Zanzibar Heroes na shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji.

Dkt. Shein ametoa zawadi hizo katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Zanzibar Heroes baada ya kufanya vizuri katika michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

“Mmeonyesha kwamba mnaweza soka katika michuano ya CECAFA, kama serikali inabidi tuwatunuku zawadi, jumla mko thelathini na tatu pamoja na wachezaji na viongozi wa timu, kwa hiyo natoa pesa shilingi milioni tatu na kiwanja kwa kila mmoja wenu na viongozi, na viwanja vyote vitakuwa sehemu moja mtaanzisha kijiji chenu,” alisema Shein.

Zanzibar Heroes walimaliza katika nafasi ya pili katika michuano ya CECAFA, huku wakiwa na rekodi nzuri baada ya kumtoa bingwa mtetezi Uganda na kuwafunga ndugu zao Kilimanjaro Stars.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: