Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema(shati jeupe) Alan Augustine na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo, Beatrice Kinabo wakikata utepe kuzindua duka la Sengerema mkoani Mwanza jana, Meneja Mauzo mkoa wa Geita Lugutu Lugutu akishuhudia.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema(kushoto) Alan Augustine akibadilishana mawazo na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo Beatrice Kinabo, baada ya kuzindua duka la Tigo mjini Sengerema.
Wananchi wa Sengerema wakishuhudia uzinduzi wa duka.
Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo, Beatrice Kinabo, akizungumza na wakazi wa Sengerma wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo jana.
Meneja Mauzo Tigo mkoa wa Geita ambaye anasimamia hadi Sengerema Lugutu Lugutu, akizungumza na wakazi na wafanyakazi wa Tigo mjini Sengerema wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
Wakazi wa Sengerema mjini na maeneo ya jirani, wakiangalia simu zitakazokuwa zinauzwa ndani ya duka hilo wakati wa uzinduzi jana
Wananchi wa Sengerema wakishuhudia uzinduzi wa duka.

*Duka hilo kurahisisha na kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa simu


*Yazindua promosheni ya ‘Back to school’ mahsusi kwa wateja wa Kanda ya Ziwa

Katika mwendelezo wa juhudi zake za kuboresha huduma kwa wateja wa simu nchini, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo leo imezindua duka jipya la kisasa mjini Sengerema, Wilaya ya Geita.

Duka jipya ya Tigo mjini Sengerema lipo kwenye barabara ya Geita, mkabala na kituo cha mafuta cha Tabasamu. Duka hilo lina uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 660,000 wa Tigo katika mji wa Sengerema na viunga vyake.

Akifungua duka hilo la kipekee, Meneja Huduma kwa Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Beatrice Kinabo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ali Maswanya alisema kuwa duka hilo jipya linaleta huduma zote za Tigo chini ya mwavuli mmoja na karibu zaidi na wakaazi wa Wilaya ya Sengerema.

‘Hiki ni kipindi ambacho TIGO kanda ya ziwa tunafungua maduka yetu mapya 6 (sita), hivyo kufanya idadi kamili ya maduka ya Tigo katika ukanda huu kufikia 15. Maduka yetu yote ni ya kisasa na yana kaunta nyingi zaidi za kuhudumia wateja pamoja na sehemu ambayo itawawezesha wateja wapya kujaribu bidhaa na huduma bora za Tigo,’ alisema Kinabo.

Alibainisha kuwa Tigo pia inazindua kampeni ya ‘Back to School’ mahsusi kwa wakaazi wa Kanda ya Ziwa, ambapo wateja watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za shule kila watakapotumia huduma mbali mbali muhimu zinazopatikana katika maduka ya Tigo. Huduma hizi ni pamoja na kununua laini mpya, kurudisha laini iliyopotea, kununua smartphone aina ya tecno S1 na R6 pamoja na kujiunga na huduma za Tigo za malipo ya baada.

‘Tumewasilikiza wateja wetu na tunazidi kuleta huduma bora karibu zaidi nao. Pia tunapanua na kuboresha huduma zetu kwa kufungua vituo vipya vya minara, kuongezea uwezo vituo vilivyokuwepo kwa sasa kwa viwango vya 3G na kasi ya juu ya 4G na pamoja na kusambaza huduma za mtandao wa simu katika maeneo ambayo zamani hayakuwa yamefikiwa na huduma za simu za mkononi. Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anafurahia faida kubwa zinazotokana na kuwa sehemu ya ulimwengu wa kidigitali,’ Kinabo aliongeza.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Alan Augustine alisema hii fursa kwa wakazi wa Sengerema kuweza kupata huduma za mtandao uliobora wa Tigo kwa kuweza kujipatia huduma mbalimbali zitolewazo na Tigo kwa ukaribu, hii inaonesha jinsi gani Tigo inawajali, “mimi mwenyewe ni mtumiaji mkubwa wa Mtandao wa Tigo hii inaweza kuturahisishia sisi wakazi wa Sengerema kutokwenda umbali mrefu kufuata huduma za mtandao,” alisema Augustine

Wateja wa Tigo katika Kanda ya Ziwa na hasa wale wanaoishi katika wilaya ya Sengerema wameelezea furaha yao kwa kufunguliwa kwa duka hilo kwani wanaamini litaboresha upatikanaji wa huduma kwa wateja.

‘Zamani tulikuwa tunalazimika kusafiri mwendo mrefu ili kupata suluhisho la huduma mbalimbali za simu. Tunafurahi na kuwashukuru Tigo kwa kusikiliza na kujibu kilio chetu cha muda mrefu kwa kufungua duka karibu zaidi na nyumbani,’ Juma Mabula, mkaazi wa Sengerema alisema.

Tigo ndio mtandao uliojizolea sifa kuu ya kuelewa mahitaji ya wateja wake na kuhakikisha kuwa wateja wote wanapokea huduma bora, za haraka na uhakika kwa viwango vya kimataifa katika maduka yake 75 yaliyoenea nchi nzima.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: