wachezaji wa timu ya marsh Academy wakifanya mazoezi katika uwanja wa Mirogo jijini Mwanza.

Timu ya Marsh Academy ya jijini Mwanza imeanza maandalizi ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni kwenye uwanja wa Nyamagana.

Hivi karibuni BMG ilishuhudia wachezaji wa timu hiyo wakifanya mazoezi katika uwanja wa Mirongo wa jijini hapa.

Akizungumzia maandalizi hayo, Mjumbe Kamati Tendaji wa timu hiyo Amiry Musso alisema atahakikisha wanafanya vizuri katika ligi hiyo kutokana na kauli mbiu yao ya kufanya vyema, kwani kikosi kimejitosheleza kwa ajili ya mashambulizi.

“Katika msimu huu wa 2017/18 tumejiwekea mikakati ya kufanya vizuri katika ligi daraja la tatu, kwani siku njema huonekana asubuhi na lengo la mazoezi hayo ni maandalizi tu, nawaomba wachezaji kufuata maagizo kutoka kwa viongozi wao ,”alisema Musso.

Naye Mchezaji wa Timu hiyo, Frank Kulwa alisema atahakikisha anaisaidia timu kufanya vizuri katika ligi hiyo, ili iweze kupanda daraja.

Kulwa alisema, atafuata maelekezo ya walimu pamoja na kuweka juhudi kwa kufanya mazoezi binafsi ambayo yatasaidia kufanya vizuri.

Alisema ni vema kila mchezaji kujiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku kwani mpira ni ajira kama ilivyo kazi nyingine na kwa sasa unalipa tofauti na zamani.

Na wakati huo huo Kulwa awaomba wadau na wapenda soka mbalimbali mkoani hapa, kujitokeza kuuunga mkono na kusaidia timu changa ambazo zinawachezaji wenye vipaji, ili waweze kufikia ndoto zao, pamoja na serikali kuhakikisha inatatua changamoto ya viwanja.

Hii ni kutokana na wadau pamoja na serikali kuwekeza na kuangalia timu kubwa ambazo zinawachezaji waliofanikiwa na kusahau wa chini ambao ndio msingi wa kufanya vizuri katika mchezo huo.

Pia aliwaomba wachezaji wachanga kujitoa katika kushirikj ligi mbalimbali ili kuonyesha vipaji na kuacha kutegemea kupata vitu vikubwa.

Hata hivyo alisema, ili soka la mkoa wa Mwanza, liendelee, viongozi, wanachama, wachezaji na wadau wanatakiwa kishirikiana na kuwa wamoja na kuacha majungu, chuki na dharau.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: