Ni rahisi tu, fanya yafuatayo:

1. Bishia nauli uliyotozwa kuwa si halali. mfano kama unakokwenda ni Dar-Mafinga, nauli inapaswa kuwa 20,000 wewe ukatozwa Dar-Njombe 25,000, bishia. Kondakta akikataa lipa, ingia kwenye gari.

2. Atakupa tiketi imeandikwa Dar-Mafinga 25,000 au atakupa tiketi imeandikwa Dar-Njombe 30,000. Pokea

3. Ipige picha hiyo tiketi, au iscan kisha itume kwenda nambari 0682 887722(kwa whatsapp, telegram au wechat) ukielezea kuwa umetozwa nauli kubwa kuliko umbali wa safari au umepandishwa bus ordinary wakati wewe ulitozwa nauli ya luxury. Na kwamba kondakta amekataa kukuandikia tiketi ya unakokwenda badala yake akakuandikia tiketi inayoonesha kituo ambacho basi linaishia. Au Tuma ujumbe au piga simu kwenda 0800 110 019 au 0800 110 020 (bure). Namba hizi tumia hata pale gari inapokatisha ruti au kuwatelekeza njiani baada ya kuharibika.

4. Basi litasimamishwa kituo cha mbele, utarudishiwa nauli yako. Kama limekamatwa na askari polisi basi dereva au kondakta atarudisha nauli na 30,000 itamhusu. Akikamatwa na SUMATRA basi atarudisha nauli na faini ya sh.250,000 itamhusu. MFANO safari yako ni kutoka DAR kwenda Mwanza nenda katika sehemu ya message andika NAULI DAR MWANZA TUMA KWENDA NAMBA 15276 NDANI YA MUDA MFUPI UTAPATA JIBU HAKIKISHA UNA SALIO LA KAWAIDA WALAU TSH 300. MTANDAO WOWOTE MESSAGE ZA KUJIUNGA HAZITUMIKI HAPA JIBU LITAKUWA HIVI

Nauli yako kutoka DAR ES SALAAM kwenda MWANZA kupitia DODOMA kwa daraja la Ordinary ni 42600, na kwa daraja la Semi Luxury ni 61400.Umbali wa safari ni kilometa 1154. Asante kwa kutumia SUMATRA MOBILE.

5. SAMBAZA UJUMBE HUU KADIRI UWEZAVYO, MUELIMISHE MWENZIO

KWA HISANI YA RSA TANZANIA,

USALAMA BARABARANI JUKUMU LETU SOTE
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: