Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi stadi VETA Sitta Peter akizungumza na wanahabari kuhusiana na umuhimu wa watanzania kutilia mkazo masuala ya ufundi stadi kwani yana nafasi kubwa ya kujiajiri na kuacha kusubiri ajira kama fani zingine leo Jjini Dar es Salaam.

Msanii wa Vichekesho MC Pilipili akipata maelezo mbalimbali ya namna mafunzo ya ufundi stadi yanavyoendeshwa na Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi VETA leo Jijini Dar es Salaam.

Msanii wa Vichekesho MC Pilipili akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake na kujionea namna Mafunzo ya ufundi stadi yanavyoendeshwa na Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi stadi VETA.


Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi stadi VETA imewataka watanzania kutilia mkazo masuala ya ufundi stadi kwani uhakika wa ajira ni mkubwa hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda.


Hayo yalisemwa leo wakati wa ziara ya msanii wa vichekesho MC Pilipili aliyekwenda kutembelea chuo hicho ikiwa ni chuo cha tano baada ya kutembelea vyuo vingine vinne tofauti.Meneja wa Mahusiano wa VETA Sitta Peter amesema kuwa suala la ufundi stadi ni la watu wote na sio kundi maalumu kama watu wanavyodhania na kuliacha nyuma wakisahau kuwa hakuna maendeleo yanayoweza kuja pasipo kuwa na wataalamu wa ufundi.


Peter amesema kuwa matumizi ya ufundi stadi yanasaidia mchango mkubwa sana katika kuinua uchumi, watu wanajiajiri na kuingizia pato taifa pasi na kusubiri kuajiriwa kama fani zingine zinavyokuwa.

"Kwa Tanzania na dunia nzima ufundi stadi soko lake linakuwa kutokana na uhitaji wa wataalamu kuelekea kwenye uchumi wa viwanda na fursa nyingi zinapatikana huko",amesema Peter.

MC Pilipili kwa upande wake amesema VETA wanafanya kazi kubwa sana ya kutoa mafunzo ya fani mbalimbali na amejionea hilo leo katoka vyuo vyote alivyotembelea.

Mc Pilipili aliweza kutembelea sehemu mbalimbali za chuo hicho na kupewa maelezo mbalimbali ya namna kazi za ufundi stadi zinavyoendeshwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: