Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kusadia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita, uliotolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Vodacom Tanzania (Vodacom Tanzania Foundation) pamoja na Taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation). hafla hiyo imefanyika leo katika Hospitali ya Chato, Mkoani Geita.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akipokea moja ya mashine za kusaidia kupumua watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Chato, Mkoani Geita. Msaada huo umetolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya Doris Mollel. Wanaoshuhudia ni Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto) na Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Chato, Dkt. Ligobert Kalasa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mkurugenzi wa  Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia pamoja na Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akimkabidhi zawadi ya Khanga Bi. Maria Maganga ambaye ni mzazi aliyekuwa katika Wadi ya Wazazi ya Hospitalini hapo.
Mkurugenzi wa  Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akimsalimia mmoja wa watoto waliozaliwa katika Hospitali ya Chato, Mkoani Geita leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa  Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) pamoja na Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel wakipanda mti katika eneo la Hospitali ya Chato ikiwa ni ishara ya mtoto anayezaliwa na kutunzwa katika mazingira bora.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: