Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akielezea lengo la kuendesha oparesheni ya kuteketeza kwa moto vifaa vinavyotumiwa na wananchi kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning'wa.Kulia ni mwandishi wa habari wa Radio Faraja na DW,Veronica Natalis - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akionesha mifugo katika bwawa la Ning'wa
Kushoto ni ng'ombe wakiingia katika bwawa la Ning'wa, katikati ni askari polisi akitoa maelekezo kwa wananchi waliokutwa katika bwawa hilo na kuambiwa waondoe mitego ya samaki iliyowekwa katika bwawa hilo.
Askari polisi akishirikiana na mwananchi kuondoa mtego wa samaki katika bwawa la Ning'wa
Zoezi la kuondoa mtego wa samaki likiendelea
Askari polisi aliyevaa kiraia akiondoa nyavu ya chandarua katika bwawa la Ning'wa.
Askari polisi wakiendelea kubomoa mtumbwi kwa kutumia nyundo
Askari polisi akimwaga mafuta kwa ajili ya kuchoma moto nyavu zinazotumika kuvua samaki katika bwawa la Ning'wa
Moto ukiteketeza nyavu
Nyavu zikiteketea kwa moto
Zoezi la kuchoma moto nyavu likiendelea
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), Injinia Sylivester Mahole akizungumza na mmoja wa wananchi aliyekutwa akifanya shughuli za kibinadamu katika bwawa hilo Jackson Kabanda
Vibanda vinavyotumiwa na wavuvi katika bwawa la Ning'wa vikiteketezwa kwa moto.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

Miongoni mwa vifaa vilivyoteketezwa kwa moto ni nyavu za kuvulia samaki, mitumbwi na vibanda vinavyotumiwa na wavuvi kujihifadhi karibu na bwawa hilo.

Zoezi hilo limefanyika leo Jumanne Disemba 19, 2017 katika bwawa hilo lenye mita za ujazo milioni 10.9 linalopatikana katika kata za Old Shinyanga, Chibe na Pandagichiza zilizopo katika wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa SHUWASA, Injinia Sylivester Mahole alisema lengo la oparesheni hiyo aliyodai ni endelevu, ni kuhifadhi vyanzo vya maji kwani bwawa hilo ni moja vya vyanzo muhimu vya maji vya mamlaka hiyo ukiachilia mbali Ziwa Victoria.

“Tumeteketeza kwa moto vifaa vilivyokuwa vinatumika kwa shughuli za uvuvi katika bwawa hili ikiwemo mitumbwi, nyavu na vibanda vilivyokuwa vinatumiwa na wavuvi,tunataka waache mara moja kufanya uvuvi hapa kwani wanaharibu vyanzo vya maji”, alieleza Injinia Mahole.

Aidha alisema shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo, uvuvi na ufugaji zinaharibu vyanzo vya maji katika bwawa hilo ambapo kina chake kimekuwa kikipungua mara kwa mara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: