Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba akiongoza kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara.Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa wizara, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Hassan Simba Yahya.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira, akizungumza na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na idara zilizopo chini ya wizara.Kulia ni Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Mwigulu Nchemba. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Kamishna Albert Nyamhanga, akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara ya polisi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna Musa Ali Musa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk. Juma Malewa akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara ya magereza kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba (hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kaimu Mkuu wa Idara Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Alphonce Malibiche, akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: