Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo viwanja vya Biafra, Dar es Salaam Januari 27, 2018.
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akiwasalimia wananchi mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam.
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza mambo mbalimbali mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wananchi kwa ujumla mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Pascal Manota akiwasalimia wananchi wa Kinondoni alipokuwa akitambulishwa kwao na kurudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM, pichani kati ni Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba na kulia kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Stephen Wasira.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Pascal Manota akirudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM, Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akiitazama kadi hiyo kwa makini.
Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassaanal ambaye hivi karibuni alihamia CCM, akimwombea kura za ushindi Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam.
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa watu waliofika kuhudhuria uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo, katika viwanja vya Biafra Kinondoni jioni ya leo.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la uzinduzi wa kampeni Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni,mapema leo jijini Dar. PICHA NA MICHUZI JR.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: