Naomba niguse mambo muhimu leo na machache maana naona wengi wetu tumezoea siasa za MATUKIO, SIASA ZA MALUMBANO na hatuitaji kusonga mbele.

Wanachadema wenzangu siasa ina vitu vitano muhimu sana navyo ni;-
1. Uvumilivu
2. Hekima
3. Busara
4. Ujasiri na mwisho ni
5. Subra

KWANINI NIMETAJA HAYA MAMBO?

Toka Jana sio baadhi ya viongozi sio wanachama wa chadema tumekosa UVUMILIVU. tumekuwa na mihemko na tumeonesha panicking kubwa inayoashiria CHUKI Kali na hata kuongea mambo bila mipaka (TUMEKOSA AKIBA YA MANENO).

Mwanasiasa Yoyote makini hatamki wala hafanyi siasa wala hazungumzi kitu kwa kupanick kwa kuona ama kusikia PICHA YA NJE tu ya jambo Fulani.

Lazima tuelewe siasa anazozifanya Lowasa sio za nguvu nyingi ila zenye akili nyingi.
Lowasa hafanyi siasa za matukio wala za kiharakati, LOWASA hafanyi mambo kwa mihemko lazima tuelewe Lowasa ni DIPLOMAT AND NOT eACTIVIST.

Lazima tuelewa kwanza alienda kufanya nini Hapo ndipo HEKIMA inaonekana, tukishajua alienda kwa mambo binasfi kama Lowasa bila kubeba title yoyote , ndipo tutoke na TUSEME ZIARA YAKE NA ALICHOKIFATA HAKUTUMWA NA CHAMA NA SIO MSIMAMO WA CHAMA.

Tusije kuwa waropokaji kwa kuzuzulisa na picha ya nje na kumbe mazungumzo yalihusu mambo muhimu ambayo labda chama kimekuwa kikiyapigia kelele kwa muda na Rais hayasikii kwa sababu alishafunga Milango ya kuwasikiliza. Hii ndio hoja ya msingi

Tunaitaji katiba mpya
Tunaitaji Tume huru
Tunaitaji haki ya uhuru wa mawazo
Tunaitaji uwanja sawa wa siasa
Tunaitaji maelewano mazuri na serikali

Lakini tunawezaje kama MIOYO YETU NI MIGUMU KUFUNGUKA KWASABABU TUMEJERUHIWA SANA???

Yesu alijeruhiwa sana na alikuwa mtenda haki lkn hata aliposurubiwa na wayahudi alisema maneno machache tu juu yao MUNGU WASAMEHE MAANA HAWAJUI WALITENDALO.

Imeandikwa na
Neema Godfrey Tz.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: