Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akifurahi kuona papai alililopelekewa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen) walipokwenda kumpa elimu kuhusu kilimo bora cha zao hilo nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange.
Dkt. Kikwete akishukuru kwa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mwanachama wa Mkikita Mtaalamu wa Kilimo cha Papai kutoka Kampuni ya Awino Farm, Ezra Machogu. Kulia ni Adam Ngamange.
Dk. Kikwete akisalimiana na Adam Ngamange wa Mkikita. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Meneja wa Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikiwete, Justine akiutambulisha ujumbe wa Mkikita nyumbani kwa Kikwete, Msoga.
Ngamange akielezea mbele ya Dkt. Kikwete kuhusu utendaji wa mtandao huo
Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra (kulia) akitoa elimu kwa Dk. Kikwete kuhusu kilimo bora cha zao hilo kwa gharama nafuu.
Ngamange akimkabihi Dk. Kikwete mafuta yaliyotengenezwa kwa kutumia mchaichai.
Mtaalamu wa Masoko na Ufungashaji wa bidhaa mshirika wa Mkikita, Murtaza Bharmal (kulia) akitoa maelezo jinsi anavyoweza kutafuta masoko kirahisi kwa kutengeneza makasha mazuri ya kuhifadhia bidhaa ili kuongeza thamani.
JK akiwa na ujumbe wa Mkikita pamoja maofisa wasaidizi wake
Dk. Kikiwete akizungumza Ngamange (kulia) pamona na Murtaza
JK akiagana na kiongozi wa ujumbe wa Mkikita, Ngamange baada ya ziara yao kumalizika
JK akiagana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Octor.

Na Richard Mwaikenda, Msoga.

RAIS mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)

Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.

Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa wakati wa mauzo.

Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.

Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.

Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo kuweka majagi mawili badala ya debe moja.

Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.

Alisema kuwa pia wamejipanga kimasoko kwa kuutumia mtandao wa Mkikita ambao tayari una watalaam wa masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na watalaamu wa kufungasha (Packaging) bidhaa kwa teknolojia ya kisasa.

Baada ya kuridhika na maelezo hayo, Rais mstaafu, alifurahi na kuishukuru Mkikita kwa kumpelekea watalaam hao kutoka Kampuni ya Awino Farm.

Ezra alizidi kumfurahisha, Dkt. Kikwete kuwa kwa heka moja akiuza papai anaweza kupata hadi sh. mil. 80,000,000.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: