Rais wa Rwanda, Paul Kagame anatarajia kuwasili nchini Tanzania kesho Jumapili, Januari 14, 2018 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika uwanja wa ndege wa Julius Kambagage Nyerere baada ya kuagana na Rais Dkt. Magufuli ambaye alikuwa akielekea visiwani Zanzibar kushiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Amani Demokrasia ya kweli, upendo na uwezo wa mkubwa wa Rais Dkt. Magufuli ndiyo msingi wa kuwavuta wageni kuja kutembelea hakuna mgeni ambaye anaweza kutembelea nchi ambayo haina upendo, amani na mshikamano. Tanzania chini ya uongozi wa Rais Magufuli inaendelea kuchanja mbuga katika nyanja za kidemokrasia hasa pia katika uwanja mwingine wa kidiplomasia na kuwafanya wageni waone sehemu nzuri ya kuja kutembelea,” alisema Makonda.

Mbali na hilo Makonda amesema kuwa Rais Paul Kagame atakapowasili atakuwa nchini kwa ziara ya siku moja na kufanya mazungumzo na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: