RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuifungua Studio ya Kisasa ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ikiwa ni shamra shamra za sherehe za Mapinduzi kutimia Miaka 54.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar(ZBC Aiman Duwe akitowa maelezo wakati wa kutembelea Studio ya kurikodia baada ya uzinduzi huo, uliofanyika katika jengo la ZBC mnazi mmoja Zanzibar leo.
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan King akitowa maelezo ya vifaa vipya vilivyofungwa katika Studio hizo wakati wa ufunguzi wake uliofanya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza wakiwa katika Studio ya kurikodia katika jengo la ZBC.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mfanyakazi wa ZBC Chumba cha kurushia matangazo ya ZBC Fatma Abubakari akitowa maelezo jinsi ya urushaji wa picha wakati wa ufunguzi wa Studio Mpya za ZBC uliofanyika leo katika jengo lao Mnazi Mmoja Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mfanyakazi wa ZBC Maimuna Said, akitowa maelezi jinsi ya kurusha matangazo kutoka chumba cha Wageni Maarufu (VIP) wakati wa kufanya mahijiano.
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC ) Aiman Duwe, akifanya mahojiano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya uzinduzi wa Studio Mpya za ZBC Mnazi mmoja Zanzibar, ikiwa ni ktika shamrashamra za kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: