Mazishi ya mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Marehemu Peras Kingunge, yamepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Janury 11, 2018 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, msemaji wa familia Bw. Omari Kimbau ametangaza.

Bw. Kimbau amesema kuwa ratiba ya mazishi hayo itaanza rasmi siku ya Jumatano jioni wakati mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwake mtaa wa Kingunge eneo la Victoria (njia ya kuelekea Mwananyamala, jirani na ilipokuwa Istana Restaurant) kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili unakohifadhiwa, na kwamba baada ya hapo kutakuwa na mkesha wa maombi.

Amesema siku ya pili, Alhamisi, shughuli zitakuwa kama ifuatavyo:

*Saa moja hadi za mbili na nusu asubuhi - Kifungua kinywa kwa waombolezaji

*Saa Tatu hadi saa Sita na nusu - Waombolezaji wataaga mwili wa marehemu

*Saa saba mchana - Misa ya marehemu kufanyika katika kanisa la St. Peters, Oysterbay.

*Baada ya misa mwili utapelekwa makaburini Kinondoni kwa mazishi.

Baada ya mazishi Bw. Kimbau ameomba waombolezaji warejee nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya chakula na kuanua tanga.

Marehemu Peras Kingunge alifariki dunia siku ya Alhamisi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. Mume wake, Mzee Kingunge, kwa hivi sasa amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha yaliyotokana na kuumwa na mbwa nyumbani kwake. Hali yake inazidi kuimarika na anatarajiwa kurudi nyumbani kushiriki katika mazishi ya mkewe wakati wowote kuanzia sasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: