WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kushoto akikabidhi fedha taslimu milioni 3 na nusu kwa ajili ya mishahara ya wachezaji wa timu ya Coastal Union ya mwezi Desemba na gharama za chakula kwa moja ya viongozi katikati anayeshughudia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union Salim Bawaziri.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kushoto akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga(TRFA) Said Soud wakati alipotembelea kambi ya timu ya Coastal Union eneo la Saruji jijini Tanga leo.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga wa nne kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Coastal Union mara baada ya kutembelea kambi yao na kuwakabidhi fedha za mishahara kwa uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya wachezaji.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga leo January 5 mwaka 2018 ametembelea kambi ya timu ya Coastal Union iliyopo eneo la Saruji Jijini Tanga ambayo hivi sasa inashiriki ligi daraja la kwanza na ipo nafasi ya tatu kwenye kundi B.

Mhe. Ummy akizungumza wakati alipoitembelea amewataka wachezaji wa timu hiyo kuongeza jitihada na kujituma ili kushinda mechi nne zilizobakia kwa lengo la kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa mwaka 2018/2019.

“Coastal Union ikipanda daraja na kucheza Premier League sio tu itawezesha vijana kupata kipato bali pia itachochea uchumi na maendeleo ya Jiji la Tanga “Alisema Waziri Ummy.

Katika kuhamasisha huko Mhe Waziri Ummy amekabidhi shilingi milioni 3 na nusu kwa ajili ya mishahara ya wachezaji ya mwezi Desemba na gharama za chakula huku akihaidi kutoa zawadi ya sh.milioni 2 kwa kila mechi watakayoshinda kati ya mechi nne zilizobaki.

Wakizungumza wakati wa tukio hilo, Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda amemuhakikishia Mh Ummy kuwa vijana wapo tayari kwa ushindi na hivyo anaamini hawatamuangusha katika michezo yao hiyo iliyosalia katika michuano ya Ligi Daraja la kwanza.

Aidha pia wameshukuru Mh Ummy kwa kujitoa kwake ili kuhakikisha timu hiyo inapanda daraja ambapo tukio hilo la makabidhiano limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA) Said Soud na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union Salim Bawaziri(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: