Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Katoro pamoja na Buseresere wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi kwenye Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimuomba Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya maeneo katika Mkoa huo.
Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi, Isack Kamwelwe akikagua baadhi ya miradi ya maji kwenye kijiji cha imalabupina wilayani Chato.
Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi, Isack Kamwelwe amewataka wakandarasi wa miradi mbalimbali ya maji kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kuwaondolea wananchi changamoto ya ukosekanaji maji ambayo imeendelea kuwakabili kwa muda mrefu .

Mhandisi Kamwelwe ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Katoro na Buseresere amesema matatizo ya maji katika miji ya Muganza, Buzirayombo na Buseresere yataanza kufanyiwa kazi na pindi tu usanifu wa mradi huu utakapokuwa tayari miradi hiyo itaanza kutekelezwa ili kumaliza kero kubwa ya maji.

Isack Saimon ambaye ni mkazi wa Buseresere amemuomba waziri kuharakisha zaidi mradi huo ambao ametoa ahadi kwa wananchi hao kwani kwasasa wameendelea kupata shida kubwa ya kupata maji na kwamba wamekuwa wakinunua ndoo ya maji kwa shilingi elfu moja hali ambayo inasababisha wasio na uwezo kushindwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Luhumbi amewasisitiza wakandarasi wote wa miradi ya maji kutumia vibarua kwa wananchi wa maeneo husika ambapo miradi hiyo inatekelezwa.

Katika Wilaya ya Chato jumla ya wananchi ambao wamekuwa wakuipata maji safi na salama ni asilimia 41.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: