Mwenyekiti Bunge kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Ndugu Suleiman Saddiq Murad akikaribishwa mapema leo Machi 6, 2018 katika ofisi za GS1 Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Fatma Kange ili kujionea utendaji kazi wao. 
Mwenyekiti Bunge kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Ndugu Suleiman Saddiq Murad (kulia) akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Fatma Kange (katikati) mara baada ya kutembelea ofisi hiyo kujifunza utendaji kazi wao.

Mwenyekiti Bunge kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Ndugu Suleiman Saddiq Murad  (kushoto) akikabidhiwa kipeperushi na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Fatma Kange (kulia)
 ili kuweza kuwatangaza zaidi.
Mwenyekiti Bunge kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Saddiq Murad  (kushoto) na ujumbe wake wakisindikizwa kuondoka ofisi za GS1 Tanzania na  Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Fatma Kange (kulia).

Na Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti Bunge kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq Murad ametembelea ofisi za GS1 Tanzania leo Machi 6, 2018 na kufurahishwa na namna GS1 Tanzania ilivyojipanga kutoa huduma zake kwa wananchi wa Tanzania. 

Mhe. Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq Murad ametoa pongezi zake za pekee kwa jinsi GS1 Tanzania ilivyojipanga kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma kwa muda mfupi.

"Nimeshangazwa kuona kuwa ukija na viambatanisho vyote unahudumiwa na kupatiwa barcodes zako siku hiyo hiyo!!!. Sikujua kwamba zipo taasisi nchini ambazo zinafanya kazi katika kasi hii," amesema Mhe. Murad.

Ameahidi kuhakikisha anawatangaza na kutoa elimu kwa wabunge wote katika kipindi cha kamati za bunge zinazoanza kazi zake hivi karibuni. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Fatma Kange amempongeza Mhe. Suleiman Saddiq Murad kwa kuweza kuwatembea na kuwa mmoja ya watumiaji wa huduma za GS1 Tanzania kwa kupata Barcodes kama mzalishaji. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: