Mwimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mbasha, ambaye alikuwa mke wa mwimbaji wa Injili Emmanuel Mbasha, amefunguka juu ya kitendo cha aliyekuwa mume wake kumlalamikia kumnyima mtoto kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Flora Mbasha amesema hawezi kulizungumzia suala la hilo kwenye vyombo vya habari au kwenye mitandao, kwani yeye ndio anaujua ukweli, na iwapo mahakama ilimpa haki ya kumuona mtoto, kuandika kwenye instagram sio sahihi kwani mahakama haipo instagram. 

“Siwezi kulizungumzia suala hilo kwenye vyombo vya habari, hilo suala kama aliandika kwenye instagram nami jibu ningelitolea instagram, na ukweli hamuujui sisi ndio tunaujua, na kama mahakama iliamua hivyo, na yeye kuandika instagram, kama mahakama iko instagram basi sawa acha aandike, ila siwezi kuliweka wazi”, amesema Flora Mbasha.

Wawili hao walitalikiana baada ya kesi aliyokuwa akituhumiwa Emmanuel kuisha na kukutwa hana hatia, na kisha Flora kuolewa na mwanaume mwengine.

Hichi ndicho alichokuwa amekiandika Mwimbaji Emmanuel Mbasha katika ukurasa wake wa instagram...
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: