Kikosi cha timu ya Township Rollers kilichovaana na Yanga na kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Kikosi cha Yanga kilichovaana na Township Rollers.
Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib akijaribu kumtoka mchezaji wa Township Rollers mchezo uliomalizika kwa Township Rollers kuondoka na ushindi wa goli 2-1 mechi iliyopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Yanga Sc imeshindwa kufurukuta dhidi ya Township Rollers ya Botswana kwa kufungwa bao 2-1 katika Dimba la Uwanja wa Taifa leo JijiniDar es salaam.

Mchezo huo ulioanza majira ya saa10:30 jioni ulianza kwa kasi kubwa huku Township Rollers wakilisakama lango la Yanga.

Wawakilishi hao wa Klabu bingwa wameshindwa kuzuia lango lao na katika kipindi cha kwanza Dakika ya 10 mchezaji wa Township Rollers Motsholetsi Sikele akiandikia Timu yake bao la kuongoza na kuwa 1-0.

Yanga nayo haikuwa nyuma katika mtanange huo Ulikuwa wa aina yake ambapo dakika ya 29 Obrey Chirwa akaisawazishia Timu yake bao mujarabu na kuwa sare 1-1 katika kipindi hicho cha kwanza na kuamsha Shangwe za mashabiki.

Katika kipindi cha pili cha mchezo huo uliokuwa wa kuvuta nikuvute kati ya timu hizo mbili zilianza kwa kasi na kukamiana ikiwa kila moja ikitafuta goli la kuongoza.

Yanga SC walizidiwa nguvu na Township Rollers dakika ya 85 mchezaji Lemponye Tshireletso aliiandikia timu hiyo bao la kuongoza na kuwa 1-2.

Kocha Msaidizi wa Yanga SC Shadreck Nsajigwa amesema wamejua makosa na watayafanyia kazi ili kuhakikisha wanafanyaje vizuri ugenini.

"Tumepoteza goli 1 lakini tutafanya vizuri ugenini kuhakikisha kilichotukwamisha ni kwamba wao wakiwa wakishuka sisi tunachelewa kupanda"amesema Nsajigwa.

Mchezo wa maruadiano unatarajiwa kuwa kati ya tarehe 14 hadi 17 ya mwezi huu ambapo Yanga wanatakiwa kushinda ushindi wa aina yoyote ili kuweza kuvuka na kuingia hatua ya makundi klabu Bingwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: