Muigizaji wa filamu Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange anatarajia kuagwa Jumapili ya Aprili 22, 2018 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam huku akitarajiwa mwili wake kusafirishwa kupelekwa jijini Mbeya kwa maziko.

Taarifa za kufariki dunia kwa video queen hot zaidi  nchini na muigizaji wa filamu Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange zilisambaa mapema jana mchana.

Ni ngumu kuamini kama Masogange amefariki dunia lakini huo ndio ukweli. Najua itakuchua dakika kadhaa kutafakari kifo cha binti huyo mwenye urembo wake na aliyejaaliwa kuwa na mvuto kwa mwenye kuona.

Taarifa kuhusu kifo cha Masogange zinaeleza amefariki dunia leo Aprili 20 , mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge Dar es Salaam. Masogange amefariki dunia akiwa bado binti mwenye umri mdogo tu hasa kwa kuzingatia amezaliwa mwaka 1989.

Hata hivyo haijafahamika sababu za kifo chake zaidi ya kuelezwa tu amefariki baada ya kuugua muda mfupi na kukimbizwa hospitalini hapo ingawa wapo wanaosema kifo chake kimesababishwa na shinikizo la damu.

Mwili wa Marehemu Agness Masogange umeondolewa kituo cha Afya cha Dkt Ngoma na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jioni hii.

Kifo chake ni pigo kwa Watanzaia walio wengi na hasa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kwani pamoja na kufanya shughuli zake binafsi lakini alipata umaarufu zaidi baada ya kuanza kutumiwa na wasanii maarufu katika nyimbo zao.

Ni hivi karibuni tu Masogange alitikisa vyombo vya habari nchini baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh.milioni 1.5 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili la kutumia dawa za kulevya aina ya heroine na pili kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Hata hivyo Masogange katika kipindi chote cha kesi hiyo ya dawa za kulevya hakuwahi kukanusha na baada ya kutolewa hukumu alilipa faini ya Sh.milioni 1.5 na akatangaza kuwa a furaha ya aina yake kwani alikuwa anabanwa na hata alipotaka kusafiri ilikuwa lazima apate kibali.

Hatimaye pamoja na Watanzania kumpenda zaidi Muumba wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo amemuita.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments: