Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akikagua shamba darasa la Mhe. Mchembe Mkuu wa Wilaya Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akiongea na wananchi Kijiji cha Kisitwi Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akikagua kiwanda cha mvinyo itokanayo na ndizi. Kiwanda hicho ni kati ya viwanda vipya 6 vilivyoanzishwa mwaka 2018.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo Mhe. Rahel Nyangasi akiwa kwenye shamba darasa lake la zao la Pamba.

Utekelezaji wa mazao ya kimkakati hasa Pamba msimu wa 2017/2018 kama ilivyoelekezwa na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim watekelezwa kwa vitendo wilayani Gairo.

Hayo yameelekezwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven alipotembelea Wilaya ya Gairo mwanzoni mwa wili iliyopita ili kuhamasisha kilimo cha Pamba ambapo ekari moja ya pamba unapata shilingi milioni 1.4.

Alidha Dkt. Kebwe alirudi wilayani Gairo kukagua utekelezaji wa maagizo yake ikiwemo kutembelea mashamba darasa ya viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Mchembe, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rahel Nyangasi na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Agnes Mkandya.

Mhe. Mchembe alimpa taarifa Mkuu wa Mkoa kuhusu kilimo cha pamba ambapo hekta 181 zimelimwa, pembejeo zimepokelewa ikiwemo mbegu za pamba kilo 3,996 viuadudu mililita 120 na mabomba 10.

Mbali na Pamba wilaya ya Gairo wameweza kulima zao la Korosho ekari 2,618 jumla ya miche 70,800 pamoja na zao la kahawa idadi ya miche 800 na mbegu gramu 3,000.

Pamba, Korosho na Kahawa ni mazao ya kimkakati na ya kibiashara hapa wilayani Gairo ambapo mazao hayo yatawainua na wananchi kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati kama ambavyo sera za awamu ya tano za Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza.

Mwisho wananchi wa Gairo walimshukuru sana Mkuu wa Mkoa, Dkt. Kebwe Steven kwa kazi kubwa anayofanya kuhamasisha Kilimo cha mazao ya kimkakati Wilaya ya Gairo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: