Kuna dada mmoja aliwasili kwenye kikao akiwa amevaa mavazi ambayo kiujumla yaliuonesha mwili wake ulivyo.

Boss wake alimtazama binti huyu machoni mwake kisha akamkaribisha kiti. Yafuatayo ni maneno ya Boss wake ambayo nadhani hatokuja kuyasahau daima;

"Binti, kila chenye thamani kubwa ambacho Mungu alikiumba katika huu Ulimwengu, kimefunikwa vema na ni vigumu kukiona na ni vigumu pia kukipata,

ALMASI hupatikana wapi?? Hupatikana chini kabisa ya ardhi, mbali mno, tena zikiwa zimefunikwa, zimesitiriwa vema na kulindwa,

LULU kubwa za Ufilipino hupatikana wapi?
Ni chini kabisa kwenye kitako cha bahari ya Palawani, zikiwa zimefunikwa vema na kulindwa ndani ya kokwa za kupendeza mno.

Wapi hupatikana DHAHABU?? Ni chini kabisa mwa machimbo, zikiwa zimefunikwa na matabaka ya miamba, hata kuzipata itakuhitaji ufanye bidii na utumie nguvu nyingi sana, SAWA???"

Boss akamtazama tena yule binti kisha akasema; "MWILI wako ni HEKALU LA MUNGU LILILO TAKATIFU, na ni mwili wa PEKEE, wewe ni wa thamani sana kuliko ALMASI, LULU NA DHAHABU na ndio maana ulipewa uvitawale, hivyo hata mwili wako ulipaswa usitiriwe pia, tena zaidi ya hayo madini, johari, lulu na vito vya thamani. Wewe umezidi thamani.

Boss akaongeza zaidi kwa kusema; "Kama utasitiri vizuri zaidi HAZINA zako za dhahabu, lulu na johari, basi wachimba madini WAKWELI, WENYE WELEDI na WAAMINIFU, watakuja, watafanya utafiti yakinifu kwa miaka kadhaa kisha watakuja na mashine zao kuchimba wakiwa wamefuata utaratibu sahihi wa kiserikali kabla hawajayachimba;

Kwanza, wataonana na serikali yako kuu (FAMILIA YAKO), kisha watasaini mkataba rasmi (HARUSI), wataanza kuchimba madini (NDOA KAMILI) bila kusahau kulipa kodi ya uchimbaji (KULIPA MAHARI),

Lakini, kama utaiacha HAZINA yako ya dhahabu, lulu na johari waziwazi juu ya uso wa dunia, basi utawavutia wachimbaji haramu wengi, ambao ni waongo, wakwepa kodi na wakwepa mikataba halali (wasiotaka ndoa). Kila mtu atajichukulia zana yake na kisha kuchimba atakavyo yeye, tena bure kabisa na kisha kuondoka zake.

Sitiri mwili wako vizuri ili uwavutie wachimbaji sahihi waliotayari kufuata taratibu zote halali".
∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽∽
Tuwasisitize DADA zetu, BINTI zetu, WAKE zetu na MARAFIKI zetu pia waisitiri vizuri miili yao, watapendeza tu na kuwavutia wakweli.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Kiukweli mkuu umenena, dada zetu shida tupu wanafikiri kuvaa nusu utupu ndo wanapendeza kumbe ni kujidhalilisha na kuonekana malaya,ndiyo maana wachimbaji wao wengi ni haramu kama wao dada zetu!

    ReplyDelete