- Ninasema hivyo kwanza kwa kuwianisha idadi ya Watanzania nchini na idadi ya vifaa vilivyokuwa tayari kuwahakikishia ULINZI na USALAMA raia wa Tanzania na wote waishio ndani yake.

- Pili ikiwa jeshi la Polisi lisingefanikiwa kama leo ingetia doa katika juhudi za kuvutia WATALII na WAWEKEZAJI jambo ambalo lingeipotezea Taifa pesa lukuki kuliko tunavyoweza kukadiria.

- Tatu ni wafanyabiashara na watu wote wenye shughuli zao za kuzalisha mali ndani ya Tanzania wanajenga imani kuwa jeshi letu la Polisi ni IMARA sambamba na ku threaten wote wenye NIA OVU za kuvuruga amani ya Taifa letu pendwa na kuwaondoa watu katika utulivu.

- Nne ndiyo nafasi pekee ya kuonyesha umahiri na vifaa vyetu vya Jeshi la Polisi kwa kuwa katika maonyesho ya kitaifa kama vile Muungano, Uhuru na mengineyo huwafikia walio wengi kwa runinga ila hii huwa live bila chenga, jambo hili linasaidia kuonyesha uwezo wa jeshi letu kwa raia na wawekezaji.

Hapo ni machache ila yote kwa yote ni kwamba JESHI LA POLISI linalinda Watanzania na si kwamba linajitokeza kukabiliana na waandamanaji ambao wanaweza kuleta madhara na kupelekea uvunjifu wa AMANI kwa wasio na hatia.

# TuchapeKazi !
# TuwapuuzeWatumwa !
# TanzaniaNiMimi
# TanzaniaNiWewe

==== ASANTE =====

Godwin D. Msigwa,
Dar es Salaam,
Tanzania.
27 Aprili 2018
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: