Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipongezana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Ofisi hiyo Aprili 10, 2018.
 Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja za Wabunge zinazohusu ofisi hao wakati wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Bungeni Dodoma, wa kwanza ni Bw.Erick Shitindi anayeshungulikia Kazi,Ajira, Vijana na wenye ulemavu, kulia kwake ni Prof.Faustin Kamuzora (Sera na Uratibu) kulia kwake ni Bi.Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu).
 Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja za wabunge kuhusu ofisi yao wakati wa kujadili na kupitisha Bajeti hiyo kwa mwaka wa Fedha 2018/2019.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt.Irene Isaka mara baada ya Bunge kupitisha bajeti Ofisi hiyo.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Bunge na Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Yona Mwakilembe Bungeni Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa akipongezana na baadhi ya Watendaji wa Ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya furaha ya kupitishwa kwa bajeti yao.
 Mkurugenzi wa Idara ya Bunge na Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Yona Mwakilembe akipongezana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa Bi.Flora Mazelengwe katikati ni Mhasibu Mkuu Bw.Anthony Chayeka, baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Ofisi hiyo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Manaibu wake, Mhe.Antony Mavunde na Mhe. Stella Ikupa (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Ofisi yake mara baada ya Bunge Kupitisha bajeti ya ofisi hiyo.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Flora Mazelengwe akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga nje ya Ukumbi wa Bunge.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ikiwa ni sehemu ya kupongezana kwa shughuli za utekelezaji wa masuala ya bajeti ya Ofisi. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: