Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia (CCM), akiongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, mtaa wa Msisiri A, Jumanne Mbena (kulia) kufanya ziara ya kujionea changamoto za mafuriko ambazo zimesababishwa na baadhi ya wananchi kujenga kwenye Bwawa Tengeneza lililopo eneo la Msisiri A kwa Mbunge huyo. Ziara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Kata ya Msisiri A, Msisiri B na Kambangwa jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia (CCM), akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A, Msisiri B na Kambangwa jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa bwawa Tengeneza lililopo eneo la Msisiri A.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, mtaa wa Msisiri A, Jumanne Mbena (kulia) akielezea machache mbele ya Mhe. Mtulia wakati alipofanya ziara ya kujionea changamoto za mafuriko ambazo zimesababishwa na baadhi ya wananchi kujenga kwenye Bwawa Tengeneza lililopo eneo la Msisiri A kwa Mbunge huyo. Ziara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Kata ya Msisiri A, Msisiri B na Kambangwa jijini Dar es Salaam.
Nyumba za wakazi wa eneo la Kata ya Msisiri A, Msisiri B na Kambangwa jijini Dar es Salaam zilivyozingira na maji.
Diwani Songoro Mnyonge akitoa maelezo kwake kuhusu mafuriko ambayo yamewakumba wananchi wa maeneo hayo.

Mbunge Mhe. Mtulia na msafara wae wakikatiza katika vichochoro vilivyojaa maji machafu.

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakiwa wamekaa katika nyumba zao zilizozingirwa na maji baada ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua za hivi karibuni wasijue la kufanya.

Juhudi za kupinguza maji kwa kuyanyonya kuyatoa katika makazi ya watu zikiendelea.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia (CCM), akitoa maelelezo kwa baadhi ya wataalam wa maji na mazingira baada ya kuangalia mmoja wa mitaro inayopitisha maji kata hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakiwa wamekaa katika nyumba zao zilizozingirwa na maji baada ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua za hivi karibuni wasijue la kufanya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: