Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri na majogoo wa jiji nchini England Mohamed Salaha amefanikiwa kuchukua tuzo ya mwaka ya PFA Player of the year 2017/18.

 Salah ameshinda tuzo la mchezaji bora la Shirikisho la wacheza soka ya kulipwa mwaka 2017-18.

Mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25, amemshinda Kevin de Bruyne, Harry Kane, Leroy Sane, David Silva na David de Gea katika kura iliyopigwa nwa wachezaji wenzake.

Salah amekuwa mchezaji wa 7 kutoka Liverpool kuchuku tuzo hiyo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa sana na kuisaidia timu yake kuwa katika nafasi ya tatu ya ligi ya EPL sambamba na kuwa na idadi kubwa ya magoli 31 ndani ya msimu mmoja.

Wachezaji wa Liverpool waliowahi kupata tuzo hiyo ni:

Terry McDermott 1979–80

Kenny Dalglish 1982–83

Ian Rush 1983–84

John Barnes 1987–88

Steven Gerrard 2005–06

Luis Suarez 2013–14

Mchezaji wa Manchester City Leroy Sane ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana , huku naye mchezaji wa Chelsea Fran Kirby ameshinda tuzo ya mchezaji bora mwanamke wa mwaka huu.

Lauren Hemp wa Bristol City ametajwa kama mchezaji bora kijana mwanamke wa mwaka huu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: