Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa jana jijini Dar es Salaam anayetarajia kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akimkabidhi tiketi Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa tiketi ya ndege jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari yake ya kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,kutoka kulia wapili ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Bw.Godfrey Mngereza.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(wakwanza kushoto) akifafanua kwa waandishi wa habari na wadau wa sanaa (hawapo pichani) kuhusu tuzo za The Africa Prestigious Awards jana jijini Dar es Salaam zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni kwa kueleza heshima ya tuzo hizo na Tanzania imepata heshima ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli nae kuteuliwa kuwania tuzo ya kiongozi bora Afrika,wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.

Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa akiahidi kwa Waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kukabidhiwa bendera kuwa atarudi na tuzo hata kama yeye hatopata basi ataweza na kurudi na hata tuzo ya Msanii Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika au Tuzo ya Msanii King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika au Mpiga picha Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga picha Bora Afrika katika tuzo za The African Prestigious Awards zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni,wa kwanza kulia ni Mama Mzazi wa Msanii Monalisa Bibi Suzan Lewis maarufu kama Natasha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: