Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

Rais wa awamu ya 5 wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Mgufuli kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uhuru wa habari Nchini ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma Mei 2 hadi tarehe 3 mwaka huu ikiwa ndiyo kilele chake azimisho la 25 kufanyika hapa Nchini kauli mbiu ni wajibu wa serikali vyombo vya habari haki na utawala wa sheria.

Ambapo wageni zaidi ya 300 wanatajiriwa kuhudhuria hafla hiyo wakiwepo wadau , wanahabari, wabunge na taasisi mbalimbali ambapo kimataifa Afrika inafanyika Nchini Ghana Accra zaidi ya nchi 100 zitawakilisha katika hafla hiyo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika hoteli ya Ramada Encore JIjini Dar es Salaam mwenyekiti wa taasisi ya vyombo vya habari Salome kitomari amesema kuwa katika hafla hiyo watazungumzia umuhimu wa uhuru wa habari kuwa na utawala bora kwa waandishi wa habari na wanasheria kama mahakama kuwa na uhuru wa kusimamia kesi za jinai za kuwa na uwazi kwa wanahabari vile vile na kukumbusha kutekeleza majukumu katika uandikaji wa habari kuwa sahihi.

Aidha makamu wa Raisi wa umoja wa Klabu za waandishi wa habari Jane Mihanji amesema kuwa wao kama wadau huwaweka mapoja waandishi wa habari na kuwapa mafunzo na kuwapatia vitendea kazi kama kamera na kompyuta ili kurahisishia kuweza kufanya kazi vizuri.

Mahinja amesema kutokana na uhaba wa vyumba vya habari mikoani inakuwa vigumu kupata stori kutoka nje ya Dar es Salaam hivyo wamewajengea uwezo wa mafunzo ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa rafiki katika utendaji.

"Tumeshuhudia stori ikiwa inatoka lakini katika kufufua maovu yanayotendeka inaleta misuko suko tunaomba serili kuwajibika katika kufanya kazi yake kwenye upande wa haki na waandishi wa habari kutoa taarifa i bila kupendelea mtu bila kuchukua rushwa," amesema Mahinja.

Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa amesema kuwa watashirikiana na wadau wengine kwenye tasnia ya habari kuhadhimisha siku hiyo umuhimu na wapo kwa ajili ya kuimarisha vyombo vya habari vinafanya kazi katika mazingira rafiki na kuhakikisha wanahabari kutoa taarifa makini zenye ubora kwa jamii.

Nae Afisa habari wa Umoja wa Wataifa (UN), Stella Vuzo amemalizia kwa kusema kuwa kwa sasa umoja huo unatekeleza maendeleo endelefu ifika 2030 kila nchi hupaswa kuelezea namana gani imetekeleza hili lengo na kuhakikisha kuwepo na ushirikiano kwa wanahabari kusaidia kupata taarifa mbali mbali .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: