Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mzee Jumanne Ngoma, mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, wakati wa uzinduzi rasmi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018

Na Mwandishi Wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kumpatia pesa kiasi cha Tsh. Milioni 100, Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite, mzee Jumanne Ngoma imsaidie katika matibabu ya ugonjwa wake unaomsumbua wa kupooza.

magufuli amesema hayo leo, Aprili 6, 2018 katika eneo la Simanjiro ambako anazindua Ukuta uliojengwa kuzungushiwa Migodi ya Tanzanite, Mirerani ili kuzuia utoroshwaji wa madini hayo.

“Madini haya yalivumbuliwa na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na kupeleka sampuli kwa Geologist (mtaalam wa miamba) kwenda kuyapima, pamoja na kutambuliwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwenye barua aliyoisani Oktoba 8, 1980 akitambua kazi nzuri ya mzee Ngoma.

“Hata alipoyavumbua hakujua yatakuwa na thamani kubwa kiasi hicho, lakini mzee Ngoma hakufaidika chochote, sasa naambiwa amepooza, nitampatia shilingi milioni 100 zikamsaidie katika matibabu,” alisema Magufuli.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: