Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana Aprili 26, 2018 ameupandisha hadhi mji wa Dodoma na kuwa jiji, huku akimtaja Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wa sasa kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo jipya.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wananchi walioweza kujitokeza katika viwanja vya Jamhuri vilivyopo Dodoma ambapo ndipo zilipofanyikia sherehe za miaka 54 ya Muungano kitaifa.

"Azma ya serikali kuhamia Dodoma ipo pale pale hakuna kurudi nyuma na tayari zaidi ya watumishi 3800 wameshahamia na mimi kama nilivyo ahidi mwaka huu nahamia Dodoma. Dodoma ndio makao makuu kwa hiyo kuanzia leo kwa mamlaka mliyonipa watanzania Dodoma ni Jiji", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "kwa hiyo maandalizi yote ya kisheria yaanze kutumika katika jiji hili jipya na hili litakuwa Jiji la pekee yake kwasababu lipo kati ya Tanzania".

Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli amewahakikishia wananchi wa Tanzania kuwa wako safi bila ya kujali vyama vyao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: