WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ''Vyandarua bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona''.Waziri Ummy akizungumza leo kwenye ugawaaji wa Vyandarua katika Zahanati ya Mwandiga mapema leo,mkoani Kigoma.

NA WAMJW-KIGOMA.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea na msisitizo wa vituo vya Afya, zahanati na hospitali za Serikali kuacha tabia ya kuuza dawa za kutibu malaria nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea zahanati ya Mwandiga iliyopo wilayani Kigoma katika kuangalia hali ya matibabu dhidi ya Malaria wilayani humo kuelekea kilele cha siku ya Malaria Duniani.

“Nawaagiza waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuweka matangazo yanayoonyesha kipimo cha haraka cha Malaria , dawa Mseto za kutibu Malaria kali ni bure kwenye kila vituo vya kutolea huduma za afya za Serikali” alisistiza Waziri Ummy.

Aidha,Waziri Ummy amesisitiza kuwa endapo mtoa huduma yeyote atakayemtoza mwananchi malipo ya matibabu na vipimo vya Malaria hatua stahiki itachukuliwa bila ya kumuonea huruma.

Waziri Ummy amesema kuwa waganga wakuu wa vituo kwa ngazi ya zahanati na waganga wakuu wa wilaya kuweka namba zao za simu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili kuwasaidia Watanzania kutoa malalamiko yao pindi wanapopatiwa huduma ambazo za hazikidhi viwango ili kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.

Waziri Ummy amesema kuwa katika kujikinga na Malaria wananchi wanatakiwa kutumia vyandarua vyenye dawa, kusafisha mazingira na kuondoa mazalia ya mbu waenezao ugonjwa huo kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Sambamba na hilo Waziri Ummy alitoa vyandarua vyenye dawa ya kukinga mbu aenezaye Malaria katika kijiji cha Mwandiga ili kuendelea

juhudi za kutokomeza Malaria nchini katika kuelekea siku ya Malaria Duniani.

Aidha Waziri Ummy ameshiriki zoezi la kunyunyizia viuatilifu pamoja na kuzindua vikosi kazi vya kunyunyizia dawa hizo ili kuua viluilui vinavyoweza kusababisha mazalia na ongezeko la ugonjwa wa malaria katika kaya mbalimbali manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani humo.

Mbali na hayo Waziri Ummy alijibu kero za wazee kuhusu vitambulisho vya matibabu ambapo alisistiza mpaka Juni 15 mwaka huu vitambulisho hivyo viwe vimepatikana kwa wazee wasiojiweza na katika Kijiji cha Mwandiga Mkoani Kigoma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema kuwa katika kuhakikisha Malaria inatakiwa kujikita kwenye kinga ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo.

Siku ya Malaria Duniani huadhimishwa kila Aprili 25 kila mwaka na maadhimisho ya Mwaka huu yatafanyika wilayani Kasulu na kauli mbiu ya mwaka huu inasema “NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: