Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uongozi wa Stand United umetishia kujitoa katika mashindano ya Azam Sports HD Federation Cup baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kuwakata mapato yao.

Hatua hiyo ya TFF imekuja baada ya kuwa na malalamiko kutoka kwa wachezaji mbalimbali wa timu za ligi kudai pesa zao za usajili au malimbikizo ya mishahara.

Akielezea hatua hiyo moja ya kiongozi wa Stand United 'chama la wana' amesema kuwa kama hawatalipwa pesa za mashindano ya FA watachukua uamuzi wa kujitoa kwani Tff imekata pesa  na  kuwalipa wachezaji wanaowadai bila kuwashirikisha.

Hata hivyo kwa upande wa Shirikisho la soka TFF wao wamesisitiza kuwa utaratibu huo wa kuzikata fedha utaendelea kwa wale wote ambao wamekiuka mikataba yao na wachezaji au makocha.

TFF haitasita kuzikata fedha klabu zote zitakazokuwa na madeni yanayodaiwa iwe kwa kukiuka mikataba yao na wachezaji,makocha au kwa namna nyingine yoyote.

Kumekuwa na klabu zinalalamika kinyume na utaratibu tunazitahadharisha kufuata utaratibu unaofahamika kinyume cha hapo hatutasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayekiuka utaratibu.

TFF inaendelea kusisitiza kwa klabu kutoa malalimiko yao kwa njia za kikanuni ili kuepuka hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi yao kama Ibara ya 50 ya katiba ya TFF inavyozungumza pamoja na Kanuni za Maadili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: