Picha ya wanafunzi wa shule ya Msingi Mapinduzi wakiwa darasani chini ya Mbuyu.

Na Mahmoud Ahmad, Dodoma.

UHABA wa vyumba vya madarasa ni miongoni mwa changamoto inayoikabili shule ya msingi Mapinduzi iliyopo kata ya Chilonwa Kijiji cha Nzali Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma ambayo hupelekea wanafunzi hao kukosa madarasa na kusomea chini ya mbuyu.

Hayo yalibainishwa juzi na Mkuu wa shule hiyo Subira Mtali Wakati wa wadau wa shirika la Action Aid walipotembela shuleni hapo wakiwa katika shughuli mbalimbali za kuelekea kilele cha maadhimisho ya Juma la Elimu Duniani.

Mtali alisema shule yake inajumla ya wanafunzi 202 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba sawa na wasichana 108 na wavulana 94 huku ikiwa na vyumba vya madarasa vinne hali inayopeleka darasa la pili kusomea chini ya mbuyu.

Aidha mkuu huyo aliendelea kwa kusema uhaba wa matundu ya vyoo pia ni changamoto inayowakabili wanafunzi hao, shule ina matundu ya vyoo sita kwa wanaume na wanawake hali inayopelea kusubiriana wakati wa kujisaidia.

‘’Halafu pia Changamoto ni kubwa vitendea kazi havijitoshelezi vitabu,tuna kopi moja moja kuanzia darasa la kwanza mpaka la tano kitabu ni kimoja kimoja unakuta na vingine hatuna kabisa mfano haiba na michezo hatuna kabisa,’’alisema.

Akizungumza katika hadhara hiyo Kaimu Afisa Elimu Wilayani hapo Amina Mussa aliwataka wazazi kuacha kuwashinikiza watoto wao kutofanya vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu na kudai kuwa watoto wa kike wanahitaji kupata Elimu sawa na watoto wa kiume.

Naye Katibu wa Jukwaa la Wanawake Wakulima wilayani hapo JUWACHA lilipo chini ya Shirika lisilo la Kiserikali ACTION AID Sophia Bhoke alisema wao kama JUWACHA walifanya tathimini ya pima kadi matokeo yake katika sekta ya Elimu waligundua uhaba wa walimu ni tatizo kwa baadhi ya shule.

“Ongezeko la wanafunzi na uhaba wa walimu imekuwa ni tatizo kubwa kwa mfano shule ya msingi Chita inawanafunzi 814 na walimu sita na Iringa Mvumi 948 na walimu nane huku shule ya msingi Mloda ikiwa na wanafunzi 1100 na walimu 10,’’aliongeza kwa kusema Bhoke.

Hata hivyo wazazi wa wanafunzi hao akiwemo Magrent Mtango alisema uhaba wa vitabu, migogoro katika Ndoa hupelekea watoto kushindwa kuendelea na shule kutokana na wazazi kutengana.

Nao wanafunzi akiwemo Elizabeth Jacob kutoka shule ya msingi Nzali alisema ukosefu wa chumba cha kujistili kwa wanawake kipindi cha hedhi inapelekea wengi wao kushindwa kufanya vizuri darasani kutokana na kutohudhuria masomo kwa wakati.

Madhamisho ya kilele cha Juma la Elimu Duniani hufanyika aprili 27 kila mwaka.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: