Watanzania wamehimizwa kujenga utamadunu wa kujisomea vitabu kwa ajiri ya kuibua fursa mbalimb ali za kimaendeleo na kuacha tab ia ya kumia vitabu kama sehemu salama ya kuhifadhia fedha kama ilivyo kwa baadhi ya watu maeneo ya vijijin na mjini huku waaadishi wa vitabu wakitakiwa kuendelea kuandika vitabu kwa lengo la kujenga taifa lenye wasomi.

Hayo yamesema na mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof, Ganka Nyamusogoro wakati wa uzinduzi wa siku ya kusoma vitabu duniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro ambapo amesema jamii nyingi za kitanzania zimejenga tabia ya kutosoma vitabu kama njia ya kuibua fursa na kuongeza maarifa baadala yake wanatumia vitabu kama sehemu ya kuhifadhia fedha jambo ambalo ni kinyume na na malengo ya waandishi wa vitabu.
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof. Ganka Nyamusogoro (wa pili  toka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa siku ya kusoma vitabu diuniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof. Ganka Nyamusogoro akikagua moja ya vitabu vilivyoonyeshwa na Chuo cha Mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani ambapo Chuo cha Mzumbe kimetoa nafasi kwa watu mbalimbali kusoma vitabu katika eneo hilo ambalo lipo maalumu kwa siku tatu chuoni hapo kuadhimisha siku hiyo ya kusoma vitabu.
 Wanafunzi wa chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro na shule ya sekondari Mzumbe wakifatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani ambaye pia ni makamu mkuu wa chuo hicho Prof. Ganka Nyamusongoro hayupo pichani.
Diwani wa kata ya Mzumbe mkoani Morogoro Recho Kungi akisisitizia wanafunzi juu ya umuhimu wa kusoma vitabu katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani yaliyo fanyika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof. Ganka Nyamusogoro ambaye alikuwa Mgeni rasmi akisoma vitabu vya tafiti vilivyofanywa na wanazuoni wa chuo Kikuu cha Mzumbe mara baada ya kuzindua hafla hiyo.
 Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro Alfred Joseph King akijisomea jarida wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani, jarida hilo limechapishwa na chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof. Ganka Nyamusogoro (katikati) akiangalia hotuba inayohusu maadhimisho ya siku ya vitabu duniani ambapo kushoto kwake ni mkuu wa idara ya huduma za wasomaji chuo kikuu cha mzumbe Sarah Mwambalaswana (kulia) ni Mkurugenzi maktaba na huduma za kiufundi chuo kikuu mzumbe Dkt. Arobogasti Musabila .
Wa kwanza kushoto ni David Onyango ambaye ni mkutubi wa maktaba ya chuo kikuu cha Mzumbe akimuonesha vitabu vilivyo pangwa katika maktaba maalumu ya madhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani wa pili kushoto Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof,Ganka Nyamusogoro anae fatia ni Diwani wa kata ya Mzumbe mkaoni Morogoro, Recho Kungi wa mwisho ni mkurugenzi maktaba na huduma za kiufundi chuo kikuu mzumbe Dkt. Arobogasti Musabila
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: