Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi simu kwa washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu 812 kwa washindi kutoka sehemu mbali mbali za nchi waliotumia namba *147*00# kununua bando za intaneti kutoka Tigo, huku kukiwa na simu 268 ambazo bado zinashindaniwa. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.
Mtaalam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi simu kwa washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu 812 kwa washindi kutoka sehemu mbali mbali za nchi waliotumia namba *147*00# kununua bando za intaneti kutoka Tigo, huku kukiwa na simu 268 ambazo bado zinashindaniwa. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael
---
Huku ukiwa imebakia wiki tatu tu kabla ya kufika kikomo cha promosheni kabambe ya Nyaka Nyaka bonus inayoendeshwa na kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania, kampuni hiyo imewahamasisha wateja wake kuchamgamkia zawadi za bure za simu janja 268 zenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 zinazopatikana kupitia promosheni hiyo.

Katika promosheni hiyo ya Nyaka Nyaka Bonus itakayofikia tamati katika wiki ya pili ya mwezi Mei, Tigo inatoa jumla ya simu janja 84 kila wiki kwa wateja wanaonunua bando za intaneti kuanzia TSH 1,000 kupitia Tigo namba *147*00#.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi za simu janja kwa washindi 47 kutoka Dar es Salaam kati ya washindi 84 waliopatikana nchi nzima katika promosheni hiyo wiki hii, Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael alisema kuwa pamoja na fursa ya kujishindia simu hizo janja, wateja wote wanaonunua bando za intaneti kupitia *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa ajili ya matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter.

‘Kupitia promosheni hii Tigo inalenga kuongeza idadi ya wateja wenye uwezo wa kufurahia huduma bora zaidi za kidigitali zinazopatikana kupitia mtandao wenye kasi ya juu zaidi na ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G. Hivyo tunawahamasisha wateja wetu wasibaki nyuma katika fursa hii ya kipekee ya kunyakua simu hizi janja zenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6,’ Woinde alisema.

Naye Wilson Chusa ambaye ni mchungaji wa kanisa la Penuel katika eneo la Mtoni Kijichi, Dar es Salaam alielezea furaha yake kwa kushinda simu hiyo ambayo alisema itamsaidia kuwasiliana na washirika wa kanisa lake kwa urahisi zaidi.

Promosheni ya Nyaka Nyaka bonus ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora ya kidigitali kupitia mtandao Tigo 4G ulioenea katika miji 22 nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: