NA DOKTA MATHEW (SHEA KWA VIJANA WENGI) 

• Ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na bateria aitwae NEISSERIA GONORRHOEAE. Ugonjwa huu hushambulia sehemu nyevu na laini za mwili (mucous membrane) ambazo ni njia zetu za uzazi kwa mwanaume na mwanammke,njia za haja kubwa kwa wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile na kooni bila kusahau macho kwa watoto wanaozaliwa kwa kina mama wenye kisonono na unaweza kusambaa na kumuua mtoto .

• Kisonono kwa mwanaume hupenda sana kushambulia sehemu ya mbele ya njia ya mkojo (anterior urethritis).

• Kwa wanawake hupenda sana kuambulia shingo ya kizazi(endocervicitis) na njia ya mkojo(urethritis)

MAKUNDI YALIYO KWENYE HATARI YA KUPATA KISONONO

• Ni vijana kuanzia miaka 15-25

• Wanaofanya mapenzi ya jinsia moja(mwanaume kwa mwanaume)

• Wanaojiuza/makahaba

• Wenye wapenzi wengi

• Matumizi mabaya au kutokutumia kondomu

• Na kama uishawahi kuumwa kisonono huko nyuma.

DALILI ZA MTU MWENYE KISONONO

KWA MWANAMKE

Wanawake wengi wenye kisonono hawana dalili kwa maana hiyo wanapata madhara makubwa ya kisonono bila ya wao kujua kwamba wanaumwa. Sehemu zinzoshambuiwa sana ni shingo ya kizazi kwa asimia 90 ikifuatiwa na njia ya mkojo kwa asilimia 800. Zingine ni njia ya haja kubwa (mkundu) kwa asilimia 40 na koo asilimia 20. Kama dalili zipo mwanake anaana kuziona kuanzia siku 7-10

Dalili ni kama zifuatazo;-

 Kutokwa uchafu sehemu za siri 

 Maumivu wakati wa kukojoa 

 Maumivu wakati wa kufanya mapenzi. 

 Kutokwa na damu isiyo hedhi mfano baada ya tendo la ndoa nk 

 Mamivu ya tumbo chini ya kitovu

KWA WANAUME

Dalili kwa wanume zinaanza mapema sana,ndani ya saa24-48 mwanauume atakua ameshaona dalili zifuatazo

Maumivu makali wakati wa kukojoa(dalili kuu)

Kutokwa na uchafu uumeni(dalili kuu)

Baada ya muda damu yawez kutoka pia

MADHARA YA KISONONO KWA WANAWAKE

Maambukizi ya mirija ya mayai na mayai(PID)

Usaha/jipu kwenye mrija wa mayai Ugumba/utasa

Kovu kwenye mirija ya mayai na kuziba mirija ya mayai

Mimba kuharibika ovyo

Maumivu ya tumbo upande wa juu kulia(perihepatitis)

Mimba kutunga nje ya mji wa mimba

Nawaomba mtag vijana wengi sana waje wajifunze.

MADHARA YA KISONONO KWA WANAWAKE

 Maambukizi ya mirija ya mayai na mayai(PID)

 Usaha/jipu kwenye mrija wa mayai

 Ugumba/utasa

 Kovu kwenye mirija ya mayai

 Mimba kuharibika ovyo

 Maumivu ya tumbo upande wa juu kulia(perihepatitis)

 Mimba kutunga nje ya mji wa mimba

KWA WANAUME

 Kovu kwenye njia ya mkojo na kuziba kwa mkojo

 Utasa/gumba

 Kuvimba mapumbu (orchitis)

 Maumivu ya viungo

Ukiachana na hizo madhara maalum za kila jinsia,usipotibu huu ugonjwa utasambaa na kushambulia moyo, macho na kua kipofu, ubongo na KIFO. Pia unakua katika hatari ya kuambukiwa magonjwa mengine hasa HIV.

MARA UONAPO DALLI HIZO HAPO JUU WAHI KITUO CHA AFYA ILI UTIBIWE NA KIZURI NA KWAMBA HUU UGOJWA UNATIBIKA.

NAMNA YA KUJIKINGA NA KISONONO

• Subiri/acha ngono.

• Uwe mwaminifu kwa mpenzi mmoja unaeaminiana naye.

• Tumia kondomu kwa usahihi.

• Wahi matibabu mara tu dalili zinapojitokeza. 

• Tumia dawa kwa kufuata malekezo ya daktari/usahihi.

• Tibiwa wewe na wenzi wako wote.

UKITAKA HABAZI ZAIDI JUU YA AFYA, MTEMBELEE DR. MATHEW KATIKA UKURASA WAKE https://www.instagram.com/doktamathew/
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: