Kuna nyakati unaweza ukawa unalalamika kwanini hauolewi, au ukimpata mwanaume anakuacha, au ndoa yako inateteleka, kumbe tatizo ni tabia zako ndizo zinakukosesha baraka zako.

Zifuatazo ni aina za wanawake ambao ni kero/chukizo kwa wanaume.

1. CHUMAULETE: Mwanamke ambaye hampi mwanaume nafasi ya kupumua, muda wote anataka pesa, story zake "Ninunulie hiki, nataka kile".
Hawa huwa chukizo kwa wanaume, na endapo atakuwa nae basi ni kwaajili ya tamaa za kimwili tu, au alimpenda sana kiasi kwamba anashindwa kumuacha, lakini bado moyoni anakuwa anasononeka juu ya huyu mwanamke.

2. DICTATOR: Mwanamke anayejifanya ana nguvu ya kutawala, yeye ndo kichwa, mwanaume ndo mkia.
Huwa hana heshima, hana utiifu, hana adabu kwa mumewe.
Mwanaume yeyote mwenye akili timamu huwa anachukia kutawaliwa, hivyo mwanamke alie mbabe, mpenda kutawala, huwa ni chukizo kwake.

3. MAMA HURUMA: Usaliti huwa haupendwi na binadamu yeyote yule, hata yule anaye saliti huwa hapendwi kusalitiwa. Wanaume huwa wanachukia wanawake wasaliti, lakini pia huwa hawana ndoto ya kuoa mwanamke mwenye tabia za umama huruma(yeyote anayetaka anampa).

4. MCHARUKO: Hawa ni aina ya wanawake ambao kelele muda wote, hawapitwi na kitu "Yuko tayari aache mtoto ndani/asimpikie mumewe sababu ya sherehe kwa jirani ", kuchambana/kusutana ndo mechi zake, kila kona anajulikana yeye, ana mazoea mabaya na wanaume wengine,
Huyu tabia za huyu mwanamke huwa ni kero kwa mwanaume wake.

5. MUCH KNOW: Mwanamke anaye jifanya anajua kuliko mumewe, mumewe akisema hivi anamuona hajui na maneno ya kejeli/dharau anayatoa.
Kila kitu anataka asikilizwe yeye tu, mumewe atakalosema/shauri linaonekana halina kichwa wala miguu.
Haambiliki, mkurupukaji, kila kitu "Niache ", hashauriki.

6. MATCHING ITEM: Hawa ni aina ya wanawake ambao anachoona fulani kafanyiwa na yeye anataka bila hata kujali uwezo wa mwanaume wake. Rafiki yake kapelekwa shopping Mlimani City, na yeye anataka, wakati huo mwanaume hana hata uwezo wa shopping ya mitumba Ilala.

7. MEMORY CARD: Ni aina ya wanawake ambao wao hawaachi jambo likapita, watalitunza na endapo utafanya kosa basi litatumika kukuadhibu. Ukifanya kosa leo, litachukuliwa kosa la mwaka 2014,2015,2016,2017, yote yataingizwa. Muda mwingine bila hata kufanya kosa, unaweza jikuta akalikumbushia na kuanza malumbano tena.

8. MWANA HISTORIA: Mwanamke ambaye anapenda kumlinganisha mwanaume wake na boyfriend/mume wake wa zamani, kama anawajua wapenzi wako wa zaman basi hata mkigombana kidogo lazima atayataja majina yao.
Anapenda kukuhukumu kuendana na historia yako, au yake.

9. POLISI: Hii ni aina ya mwanamke ambaye analinda usalama wa mwanaume wake mpaka inageuka kuwa kero.
Wivu ndio mapenzi, lakin huyu ana wivu kupitiliza, atapekua simu ya mumewe, atapenda kumfata nyuma nyuma, kufatilia kwenye vijiwe vyote anavyokaa na akimkuta ni varangati muda wote, atapenda kuuliza "Huyu nani, kwanini ulikua unaongea na flani", ugomvi ndani kila saa, kuhojiana kila wakati.

10. KISIRANI: Huyu ni aina ya mwanamke ambaye jambo dogo kanuna, mara kakasirika, kidogo ugomvi.
Hataki ndugu, hataki wazazi, hataki wafanyakazi, anataka muda wote awe yeye tu.

12. MCHOYO/MBINAFSI: Hawa wachoyo, ndo huwa tatizo zaidi.
Mfano: Ndugu wakija watashindia maembe, lakini yeye atakula na kufurahi kivyake.
Huwa anajiwazia yeye tu, vyake tu, hawazii wengine, vyake huwa vyake na vyako huwa vyake pia.

13. DAMPO: Huyu huwa ni mtihani, mchafu muda wote, hajitambui wala kujitunza. Uchafu huwa ni kero kwa mwanaume wake.

14. MTANGAZAJI: Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hana kifua, Kila jambo/mipango/siri za ndani ya ndoa yake/mahusiano yake lazima ataitoa.
Hachelewi kumtangaza mumewe kama ana kibamia, hana hela, kafanya hivi mumewe.
Akikosana na mumewe basi marafiki, ndugu, wazazi, majirani, wote watajua kama amegombana na mumewe kwasababu fulani.

Haya jichunguze wewe uko namba ngapi, na uanze kubadilika.
Aidha ili uilinde ndoa yako, au kama hujaolewa bado basi ili upate wa kukuoa atakaye vutiwa na tabia zako.

UJUMBE UMEFIKA !!!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: