Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akijibu swali kuhusu utaratibu unaotumika kutoa ajira kwa wananchi katika sekta za Muungano leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki na Naibu Waziri Mhe. Dotto Biteko leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Tate Ole Nasha akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa inajenga vyuo vya ufundi stadi kila Wilaya hapa nchini leo Bungeni Jijini Dodoma.
Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi ( kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mbunge wa Welezo Mhe. Saada Salum Mkuya akiuliza swali kuhusu utaratibu unaotumika katika kutoa ajira katika sekta za Muungano.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi akieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi na Jeshi la Ulinzi la Wananachi wa Tanzania ( JWTZ) wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakati wa kipindi cha maswali na majibu, leo Jjijini Dodoma. (Picha na Frank Mvungi- MAELEZO).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: