Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akisoma barua ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) ya kumuomba kujiuzuru nafasi hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) akisema machache ya kushukuru baada ya barua yake ya kuomba kujiuzuru nafasi hiyo kukubaliwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) akisema machache ya kushukuru baada ya kuwasilisha barua yake ya kuomba kujiuzuru nafasi hiyo kukubaliwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kumkubalia, akimshukuru na kumwombea kila la heri Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) baada ya kusoma barua yake ya kuomba kujiuzuru nafasi hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018.

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Dk.John Magufuli amesema ametafakari kwa kina na kuamua kuridhia kung'atuka kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Abdulrhaman Kinana lakini hadi atakapomaliza muda wake ndipo atapumzika.

Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na Wajumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa kwenye kikao kilichofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema anatambua juhudi kubwa ambazo zimefanywa na Katibu MKuu wao.

"Ni zaidi ya mara mbili Katibu Mkuu wetu ameomba kumpuzika lakini nikawa namkatalia na hata alipokuwa anaanzisha hoja hiyo kisiri siri mimi nilikuwa naanzisha pointi nyingine.

"Lakini nieleze tu natambua juhudi kubwa ambazo amefanya.Lakini pia nikatambua kuna makatibu wakuu wengi wamekitumikia chama chetu na wengi tu maana walikuwepo hata kabla mimi kuanza shule ya msingi.

"Natambua umri alionao Katibu Mkuu wetu.Hivyo nilimuita mzee Shein(Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) nikamueleza akaniambia mruhusu akapumzike,nikamuita mzee Mkapa naye mkubalie.Hivyo nimekubalia acha akampumzike,"amesema.

Pia amesema jana alimuita Katibu Mkuu Kinana na wakazungumza akimini huenda atabadili mawazo yake lakini bado akabaki na mawazo."Hivyo nimemkubalia akapimzike lakini atapumzika baada ya kumaliza muda wake,"amefafanua Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Magufuli.

KINANA ASHUKURU KUKUBALIWA KUPUMZIKA

Wakati huo huo Katibu Mkuu Kinana amesema kuna wakati wa kufanya kazi na wakati wa kupumzika na anaelewa ugumu ambao CCM wanaupata wa kutomkubalia.

"Naangalia nyuso zenu zinaonesha namna ambavyo hampo tayari kunikubalia lakini Mwenyekiti wetu amesema tumewahi kuwa na makatibu wakuu wengi na kweli tumekuwa na makatibu wakuu saba kabla yangu. Hivyo nakushukuru Mwenyekiti kwa kunikubalia, nashukuru Makamu Mwenyekiti kwa kunikubalia na nashukuru mzee Mangula kwa kunikubalia.

"Nakumbua kuna siku Mwenyekiti alikuja pale Lumumba na uliamua kujitoa mhanga kwani alipokuuliza kuhusu kupumzika ulimwambia anikubalie.Mwenyekiti kama alikukasirikia hivi lakini nashukuru sana maana ulinisaidia na ulijitoa mhanga,"amesema Kinana.

Amesema amekitumikia Chama hicho kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 30 lakini kwa kipind cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2013 alijitolea sana ndani ya CCM lakini hatimaye anashukuru kwa kukubaliwa kwa ombi lake na Mwenyekiti wao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: