Meneja Biashara wa CRDB Bank, Tawi la Vijana, Zaituni Manora, akitoa sera za benki hiyo kwa wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, wakati wa ufunguzi wa maonesho yao, yaliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema, Viawanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com).
Ofisa Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo akimwelekeza mmoja wa wananchi aliyefika kwenye banda la benki hiyo katika maonesho hayo, jinsi ya kujaza fomu za miamala ya kifedha ya benki hiyo.
Ofisa Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo akiwapatia maelezo baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la benki hiyo katika maonesho hayo, jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo (kulia), akimpatia maelezo mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali wa Ilala, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto), wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya huduma za kifedha pamoja na ya wajasiriamali kabla ya kuyafungua.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto), akimwuliza jambo Ofisa Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo (kulia), akiwa kwenye banda la benki hiyo, wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya huduma za kifedha pamoja na ya wajasiriamali kabla ya kuyafungua maonesho hayo.
Ofisa Huduma kwa wateja wa CRDB Bank, Makao Makuu, Richard Tangazo (kushoto), akimpatia maelezo mmoja wa wajasiriamali aliofika kwenye banda la benki hiyo, katika maonesho hayo.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akiwa meza kuu pamoja na baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Ilala kabla ya kuyafungua maonesho hayo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omar Kumbilamoto, akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kuzungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo. 
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akizungumza na wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, wakati akiyafungua maonesho yao, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Diwani wa Gongolamboto, Jakob Kisi, akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa CRDB Bank, Meneja Biashara, Tawi la Vijana, Zaituni Manora, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. CRDB Bank, ni moja ya waliodhamini na kufanikisha maonesho hayo ya wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: