Mkuu wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Senyamule akikagua mradi wa maji katika wilaya ya Same
Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akitoa maagizo ya kutaka mradi wa maji Hedaru kukamilika haraka
----
MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Senyamule amemtaka mkandarasi wa mradi wa maji Kijiji cha Hedaru kukamilisha mradi huo unaogharimu bilioni 1.18 ifikapo Mei 30 mwaka huu.

Akitoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo juzi mkuu huyo wa wilaya alisema lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli ni kuona mwanamke anatua ndoo kichwani kwa kupata huduma ya maji .

Alisema mradi huo umelenga kufikia vijiji 10 ambao ulitakiwa kukamilika toka mwaka 2015 ila hadi sasa umekuwa ukienda kwa kusuasua .

Hivyo alimtaka mkandarasi kuhakikisha maji yanatoka sasa wakati wa kiangazi kwani wananchi wamekuwa wakihofu kama kweli mradi utatoa maji wakati wa kiangazi.

"Naitaka kamati iliyoundwa kusimamia maji kukagua maeneo yote na kutoa taarifa kwa mhandisi kabla mkandarasi hajakabidhi ili akabidhi mradi usio na kasoro"

Hata hivyo alisema katika ukaguzi alioufanya katika mradi huo amebaini mifumiko mingi imevunjika, koki nyingi zimeibiwa.

"Mji wa Hedaru ni mji unaaongoza kwa kukua kwa kasi Wilayani Same Mhandisi Mussa aeleza jinsi mradi huo utakavyoongezewa nguvu na tanki lingine linalojengwa mwaka huu, ili kukidhi ongezeko la watu"

Alisema kuwa mradi huu ni kati ya miradi iliyokuwa imeainishwa kwenye ilani ya CCM 2010- 2015 hivyo atakayecheza nao atawajibishwa vikali .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: