Pichani ni upauaji wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mabui. Picha namba 5-6 zinaonyesha upigaji wa lipu unaoendelea kwenye Shule ya Msingi Mabui.

Na Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge.

Fedha za Mfuko wa Jimbo zimezidi kuboresha miundombinu ya Elimu hasa kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa Shule za Sekondari na Msingi za Jimbo la Musoma Vijijini.

Tarehe 18 Mei 2018, Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Verediana Mgoma, alikagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye Kijiji cha Mabui Merafulu, Kata ya Musanja. Akiwa huko, alishuhudia ujenzi wa vyumba vya madarasa ukiendelea kwa kasi kubwa katika Shule ya Msingi Mabui na Shule ya Sekondari Mabui.

Mafanikio hayo yametokana na upatikanaji na utumiaji mzuri na wa wazi wa Fedha za Mfuko wa Jimbo. Mchango mkubwa kutoka wa wananchi ni nguvu zao - ujenzi wa kujitolea baada ya kupewa vifaa vya ujenzi.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi, Mtendaji wa Kijiji cha Musanja na Kaimu Mtendaji Kata ya Musanja, Ndugu Emmanuel Eswaga alisema, Kata yake ilipokea mabati 108, mifuko ya saruji 60 na Tsh Mil 7 kutoka Mfuko wa Jimbo na kwa Mbunge wa Jimbo ili kukarabati majengo ya Shule ya Msingi, ikiwemo ujenzi wa vyumba vipya vinne (4) katika Shule ya Msingi na Sekonadari Mabui. Aliongezea kuwa, wao kama Serikali kwenye ngazi ya Kijiji na Kata wanajitahidi kuhamasisha ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo.

Hata hivyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mabui, Ndugu Generose Severine alisema, kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi kwenye Shule za Msingi, kumefanya wanafunzi wengi zaidi kujiunga na Kidato cha I kwenye Sekondari hiyo na kupelekea kuwepo na upungufu wa vyumba vinne (4) ambavyo sasa vinajengwa kwa kasi kubwa.

Naye Diwani wa Kata hiyo, Ndugu Elias Ndaro ameishukuru Serikali kwa kutoa Fedha za Mfuko wa Jimbo, na Mbunge wao Prof.Sospeter Muhongo kwa juhudi zake katika kuboresha Sekta ya Elimu kwenye Kata yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: