Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akisalimiana na Mzee John Steven Akhwari Mwanariadha anayeheshimika Duniani mara baada kwasili alipomtembelea nyumbani kwake Eneo la Sani mjini Mbulu mkoani Manyara jana, John Steven Akhwari aliiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika Mexco City mwaka 1968 John Steven Akwari aliyekuwa wa mwisho kumaliza mashindano ya marathon mwaka 1968 Mexico City katika mioyo ya mamilioni ya watu anakumbukwa kama shujaa ambapo mwaka 2008 katika mashindano ya Olimpiki ya Beijing nchini China miaka 40 baadaye, Akhwari aliteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Olimpiki. Katika mashindano hayo ya mwaka 1968, Akwari akiwa na umri wa miaka 30 akiiwakilisha Tanzania alikuwa mwanariadha wa mwisho (57) kumaliza mashindano kati ya 75 walioanza.

Mshindi wa mashindano hayo Mamo Wolde wa Ethiopia alitumia saa 2:20:26 huku Akhwari akimaliza zaidi ya saa moja baadaye yaani alitumia saa 3:25:27 kukiwa na watazamaji wachache uwanjani na jua lilikwisha kuzama. Awali wakati anaanza mbio hizo, Akwari alianguka na kupata majeraha kwenye goti ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya hewa ya Amerika ya kati kuwa tofauti na nyumbani. Wanariadha wenzake walimpita moja baada ya mwingine na hivyo kukatiza ndoto yake ya kuiletea Tanzania medali ya kwanza kabisa ya Olimpiki, lakini hakukata tamaa bali alinuia kumaliza hayo mashindano.

Akiwa amefungwa bandeji mguuni huku akitokwa na damu, Akhwari alitokeza uwanjani saa moja baada ya mshindi kutangazwa, na kukiwa na watazamaji wachache na waandishi wa habari na giza likianza kuingia, uwanja ulizizima kuona Akhwari anachechemea akiwa na maumivu kuelekea mstari wa kumaliza mbio, wengi waliguswa baada ya kushuhudia tukio hilo. Alipoulizwa na waandishi kwa nini aliendelea na mashindano baada ya kuumia, aliwajibu kwa utulivu jibu rahisi ``Nchi yangu haikunituma maili zaidi ya 5000 kuanza mbio, bali kuzimaliza``
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akisalimiana na Mzee John Steven Akhwari wakati alipoongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliyemtembelea mzee huyo nyumbani kwake eneo la Sani mjini Mbulu.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza jambo na Mzee John Steven Akhwari.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Mee John Steven Akhwari alipokuwa aktoa maelezo kwake kuhusu mbambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya katika masuala ya mchezo wa Riadha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakiangalia tuzo mbalimbali ambazo Mzee John Steven Akhwari kulia aliwahi kutumikiwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakionyeshwa mwenge wa Olimpiki ambao Mzee John Steven Akhwari kulia kutumikiwa jijini Beijing China baada ya kuukimbiza akiwa Balozi wa Mashindano hayo mwaka 2008.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyeshwa moja ya tuzo ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa nchini Uswisi .
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyesswa Nisahani ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi
Hapa wakionyeshwa vyeti mbalimbali ambavyo Mzee John Steven Akhwari aliwahi kutunikiwa kutambua mchango wake katika mchezo wa Riadha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga wakiwa katika picha ya pamoja na Mzee John Steven Akhwari mara baada ya mazungumza yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: