Shirika la Kimarekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) la Kukuza Biashara na Uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki (East Africa Trade and Investment Hub) limezindua Taarifa ya Tathmini ya Sera za Uwekezaji za Tanzania kwa mwaka 2018 (Tanzania Investment Policy Assessment 2018) ikiwa ni sehemu ya Jukwaa la Marekani na Tanzania lililoangazia Sera na Ubunifu lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Tathmini hii itawasaidia watengeneza sera, wakala wa mabadiliko na wawekezaji wanapofanya kazi pamoja kuhimiza, kuchochea, kulinda na kuongeza zaidi kiwango cha uwekezaji wa wawekezaji kutoka nje (FDI) nchini Tanzania.

“Kwa kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, Tanzania inaweza kutatua changamoto zake za kimiundombinu na kukidhi mahitaji yake kama vile upatikanaji wa nishati ya gharama nafuu kwa wote na uendelezaji wa mtandao wa usafirishaji na wakati huo huo ikijenga uwezo wa watu wake, ambao ndio watakaoifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na hata kupiga hatua kubwa zaidi ya hapo," alisema Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dr. Inmi Patterson.

Serikali ya Marekani imedhamiria kwa dhati kushirikiana na Serikali na watu wa Tanzania ili kuimarisha na kuboresha mazingira ya kisheria na kiusimamizi wa uwekezaji kutoka nje ili kujenga Tanzania imara na yenye ustawi zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: