Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewasilisha baurua ya pongezi kwa katibu mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally aliyeteuliwa kuongoza chama Hicho.

Barua hiyo ya Maalim ambayo imewasilishwa saa chache tu na Msaadizi wake Mbaralala Maharagande mara baada ya kumalizika shamrashamra za kukabidhiana ofisi baina ya aliyekuwa katibu mkuu wa zamani. Maharagande amesema barua hiyo amesema mara baada Dr. Bashiru Kuteuliwa kuwa katibu Mkuu mpya wa CCM ndipo Maalim ameandika barua ya kumpongeza.

“Katibu mkuu wa chama chetu ameandika barua kumpongeza Dkt Bashiru na Kumpongeza Kinana kwa kuweza kuimarisha demokrasia ya vyama kwa kipindi chote alichokuwa akiongoza CCM kwa kujali maslahi ya nchi kwanza kuliko mambo binafsi ya chama”amesema Maharagande.

Amesema Dkt Bashiru ni moja ya wasomi watakaoleta mabadiliko katika mfumo huu wa vyama vingi licha ya kuwa si vyema kutabiri atakachokifanya kwani watu wajue tu kuwa kiongozi huyu ni mzalendo ambaye anaamini katika mabadiliko makubwa katika masuala ya kisiasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: