Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo (kulia) akimkabidhi Jeremiah Mwamlenga (kushoto) zawadi ya simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama moja wa washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo. Jumla ya washindi 996 wamepatikana katika prmosheni hiyo inayoendelea.
Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo (kulia) akimkabidhi Mwanaisha Bakari (kushoto) zawadi ya simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama moja wa washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo. Jumla ya washindi 996 wamepatikana katika prmosheni hiyo inayoendelea.
Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo (kulia) akimkabidhi Nuhu Munhambo (kushoto) zawadi ya simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama moja wa washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo. Jumla ya washindi 996 wamepatikana katika prmosheni hiyo inayoendelea.
Picha ya Pamoja.

*Wateja 996 wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za data bure 

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, imewazawadia washindi 996 kutoka sehemu mbali mbali nchini simu za zenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus

Akikabidhi zawadi kwa washindi 11 jiijini Tanga leo, Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo alibainisha kuwa kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.

‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na mahitaji ya wateja na utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora za mtandao wa Tigo 4G wenye kasi zaidi na ulioenea zaidi nchini,’ alisema.

Katika promosheni hiyo murwa ya Nyaka Nyaka Bonus, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wanapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na hayo, wateja pia wanapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 ambazo zinatolewa bure na Tigo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: