Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na Maria na Consolata leo kabla ya kuanza safari ya kwenda Iringa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai na wengine ni wataalamu waliokuwa wakiwapatia matibabu pacha hao.
Kulia ni machine ya CPAP & Oxygen ambayo Maria na Consolata wamepewa endapo watahitaji matibabu yanayotolewa kwa kutumia mashine hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwaaga Maria na Consolata leo.
Maria na Consolata wakisaidiwa kuingizwa kwenye gari ikiwa ni safari ya kuelekea Iringa leo. Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imewaruhusu Maria na Consolata waliokuwa wamelezwa katika hispotali hiyo kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na afya zao kuimarika.

Pacha hao walikuwa wakipatiwa matibabu na madaktari bingwa wa Muhimbili na leo wamepelekwa Iringa ambako watapokelewa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema pacha hao wamesindikizwa na madaktari wa Muhimbili haid Iringa na kwamba wakiwa huo wataendelea kupatiwa matibabu.

“Consolata na Maria tumewaruhusu leo. Hii ni baada ya madaktari kujiridhisha kwamba afya zao zimeimarika. Wataalamu wetu wamewafanyia vipimo mbalimbali na pia tumewasiliana na wenzetu wa nje na tukakubaliana tuwaruhusu sasa,” amesema Prof. Museru.

Prof. Museru amesema kwamba pacha hao wamepatiwa machine ya CPAP & Oxygen ambayo itawasaidia kuwapatia tiba endapo watahitaji wakati wakiwa Iringa.

Wakizungungumza kwa nyakati tofauti, Consolata amesema kwamba Muhimbili imewapatia huduma nzuri na wanawashukuru wataalamu mbalimbali waliokuwa wakiwapatia matibabu tangu walipolazwa.

Naye Maria akizungumza kwa furaha amesema hivi sasa anajisikia vizuri tofauli na awali-kabla ya kupelekwa katika hispotali hiyo kwa ajili ya matibabu. Pia, amemshukuru mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili kwa kuwapatia huduma bora za matibabu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: