WAZAZI na Walezi mkoani Tanga wametakiwa kuhakikisha wanawapa watoto wao zawadi kwenye kpindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuwaingiza kwenye mpango wa Toto Afya Kadi ili waweze kunufaika na matibabu wakati wanapougua.

Hayo yamesemwa na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens (Pichani) ambapo amesema zawadi hiyo ni muhimu sana katika ukuaji wao badala ya kuwanunulia nguo ambazo wanavaa kwa wakati Fulani na baaadae kwisha.

Amesema mpango huo ni muhimu kwa watoto wao kutokana na kuwahakikishia kupata huduma za matibabu wakati wote wanapokumbana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuathiri.

“Ndugu zangu wazazi na walezi kwenye kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani zawadi mzuri ambayo mnaweza kuwapatia watoto wenu ni kuwaingiza kwenye mpango huu wa Toto Afya Kadi kwani malipo yake yana muwezesha mtoto kupata huduma za matibabu mwaka mzima kwa kiasi cha sh.50,400” Alisema.

Hata hivyo amesema wataendelea kuhimiza wananchi kuweza kuwaingiza watoto wao kwenye mpango huo ili waweze kuwahakikishia watoto wao kupata huduma za matibabu bila vikwazo hasa wanapokuwa wakiumwa .(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: