Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisisitiza kuhusu sekta ya fedha kuwa na mikakakati yenye tija katika kukuza uchumi wa viwanda wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, akielezea kuwapo kwa changamoto ya kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma za bima za kilimo na gharama kubwa za huduma za fedha wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Kaimu Kamishna wa Sera za Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Michael Nyagoga akielezea dhana ya Mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango kuwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za
kifedha za Sekta ya Viwanda nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, akisikiliza kwa makini wito wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga (hayupo pichani) kuhusu Sekta ndogo ya Benki kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda, Jijini Dodoma.
Baadhi ya wakurugenzi wa taasisi za fedha na maafisa waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani) alipokua akieleza wajibu wa sekta ya fedha nchini katika kuwezesha viwanda vidogo vidogo, wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Wakuu wa taasisi za fedha wakiwa katika majadiliano na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma kuhusu mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa viwanda nchini.
Wakuu wa taasisi za fedha wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma ulioangazia mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa viwanda nchini. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizaya ya Fedha na Mipango)

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma.

SERIKALI imeitaka Sekta ndogo ya Benki kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda na kilimo pamoja na wajasiriamali wadogo.

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, katika Mkutano wa wadau wa Sekta ya Fedha uliowashirikisha wabunge, washirika wa Maendeleo, wakuu wa Taasisi za fedha na Wizara ya Fedha na Mipango.

Prof. Luoga alitoa wito huo kufuatia kuwepo kwa changamoto katika Sekta hiyo ikiwemo ukosefu wa uwekezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika viwanda, kilimo na miundombinu pia ukosefu wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

“Kuna kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma za bima za kilimo, gharama kubwa za huduma za fedha, mifumo hafifu ya kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha, ukosefu wa elimu ya fedha kwa wananchi na wananchi wengi kutofikiwa na huduma za fedha ambapo ni asilimia 8.6 tu ya nguvu kazi ya wananchi waishio vijijini wanapata huduma za benki ikilinganishwa na asilimia 32.1 ya nguvu kazi kwa wanaoishi mijini” alisisitiza Prof Luoga

Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo, Serikali ilifanya maboresho ya Sekta ya Fedha katika eneo la ubinafsishaji wa benki za Serikali kurekebisha na kutunga sera na sheria mbalimbali hadi kufikia Desemba, 2017 ili kuweka misingi imara ya kuwezesha ukuaji, ushindani na ufanisi katika sekta ya fedha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: